Tuliowahi kukopesha watu pesa na tukazimwa tukutane hapa

Wewe jamaa una roho ngumu sana. Hiyo inaitwa komesha watoto.
 
Yap alinihisia ila hakujua kama mimi mwenyewe ndio niliingia mchezoni yeye alikuwa anahisi labda nilituma mateja ndiomana hata chakueleza hakuwa nacho
Pengine wala hakukuhisi wewe. Mtu kama huyo lazima kutakuwa na watu wengi tu wanamdai na anawazungusha. Kwahiyo hapo hakujua mhusika ni nani. Au alihisi ni KARMA pia.
 
Pengine wala hakukuhisi wewe. Mtu kama huyo lazima kutakuwa na watu wengi tu wanamdai na anawazungusha. Kwahiyo hapo hakujua mhusika ni nani. Au alihisi ni KARMA pia.
Yap yawezekana
 
Sitamsahau mligo na masiva
 
Hehehehheeee. Kuna mwana mmoja ivi tumesoma wote O'level. Yy hakuendelea mbele akawa mtu mishe town.

Basi bwana mm 2nd yr nkataka nipange gheto na mda huo nilkua field so sikuwepo mjini. Nkachonga na mwana anitafutie gheto mjini nimtumie hela.

Jamaa akaniambia gheto lipo ila kupitia kwa dalali...nkasema poa. Mm dalali simjui nakutumia ww. Akasema poa. Nkamtumia hela ya chumba na dalali. Kumbe mhuni amechonga na wahuni wenzie wa ekt dalali.
Wakawa wamenipiga hela kiivo.

Badae figisu zikaanza. Nkawa napiga simu wananipotezea. Nkawa namsumbua yule jamaa anaejiita dalali. Ikabid afunguke ...ananipa siri kua hakuna cha chumba wala nn na yy sio dalali bali alikodiwa tu.

Basi nkawa nimepata ukweli. Gheto tulipanga tukakae na washkaj zangu ivi.

Akaanza kudai kua alimpa hela dalali ila analeta mizengwe.
Basi bwana mm nkajifnya fara nkamwambia hela yenyewe ya njaa, kwanza mm nna miradi mingi inayoniingizia pesa na boom limetoka kutema tu juzi. Ahahahahahah πŸ˜‚πŸ˜πŸ˜πŸ˜.

Nkampanga tuktane tukatanue mjini siku mingi hatujaonana. Heheheheh watu wa mjini wanavyopenda ofa vya bure. Si akakubali tuonane. Heheheheeh.
Nkmwambia "T" muhuni wangu mmoja ivi ambae ndo tulkua tunaenda kukaa wote gheto tukazama mtaa wa kuktana.

Kweli bhna jamaa akawa amekuja. Tukaingia restaurant moja iv ktukaanza kupiga vyombo. Chips, soda,samaki, bia. Kula kwa Fujo mingi mingi.

Kabla bill haijaja, kwa kutabasam nkaanza kusifia simu yake kua nzuri. Baadae nkamuomba niiangalie.

Alivyoitoa tu kunipa, nkaanzisha stori za kodi ya nyumba waliyokula. Simu nkampasia mhuni wangu T.

Heheheheh.jamaa kahahaha. Nkampgia yule jamaa ake, akamchana kua J wape hela washkaj. Timbwili timbwili watu wakajaa. Jamaa wakamharass atoe hela la sivyo aende polisi. Jamaa akakubali kutoa hela iliyokua kweny simu. Akaomba simu akachukua pesa akatutumia kwenye simu yetu.

Heheheheheh. Case solved...bill yake akalipa mwenyewe. πŸ˜‚πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜πŸ˜πŸ€ΈπŸΎπŸ€ΈπŸΎπŸ€ΈπŸΎ.
Nilicheka sana ujanja wa yule πŸ’
 
Unavyomkopesha mtu inamaana hana kitu sasa unategemeaje mtu uliyemkopesha hana kitu akulipe baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…