TULIOWAHI KULALA LOCKUP/SELO TUKUTANE HAPA

TULIOWAHI KULALA LOCKUP/SELO TUKUTANE HAPA

Kuna harufu mbaya na mbu kibao...

Kosa langu eti ni kuendesha chombo cha moto huku nimekunywa balimi.Nilitoka club kujirusha.Traffic wanasumbua sana usiku
 
Kesi ya kipuuzi sana,

Nilikamatwa napiga picha eneo la kanisa

Mtetezi nikapata ila mkuu wa kituo akawa anabana.
Dhuuuuu Pole aiseeee mm
Ndo maana nasema hata
Nipate askar anapgiwa na nna
Uwezo wa kumuokoa wala
Smuokoi cha zaid namuongezea kipgo
 
Siji sahau siku niliwekwa ndani kisa kuendesha bajaji mpya iliotoka kushuka kwenye gari kupeleka kwa fundi kuiweka vizuri. etii kwanini natembea na bajaji isio na stika yoyote ile? nilipigwa makofi nakuwekwa ndani siku tatu pamoja na bos wangu hio 2008.
Duh,pole ndg!!
 
Dhuuuuu Pole aiseeee mm
Ndo maana nasema hata
Nipate askar anapgiwa na nna
Uwezo wa kumuokoa wala
Smuokoi cha zaid namuongezea kipgo



Dhuuuuu Pole aiseeee mm
Ndo maana nasema hata
Nipate askar anapgiwa na nna
Uwezo wa kumuokoa wala
Smuokoi cha zaid namuongezea kipgo
Dunda kabisa, ikiwezekana kata hadi malighafi za ikulu ukawape nguruwe watibu njaa zao
d112f8da8602f9c9fc507c8c19f45667.jpg
 
duh poleni sana.Mimi walitaka niingiza selo ilikua usiku nimetoka club kichwa kikiwa resi kidogo nilitembeza kichapo kwa polisi watatu alafu nikachomoka mwendo wa super sonic speed enzi hizo niko secondary,
 
Sijaingia kule ndani mara 2 natoa hela naachiwa
Tena usiku
 
Aise siwezi kusahau ilikuwa mwaka 2010 nikiwa nipo sekondari kuna mzee alikuwa na kawaida ya kutongoza wavulana siku hiyo akaniita akamwaga sera zake kilichofuata baada ya hapo nikampa majibu ya hovyo ambayo yalimuuma na rafiki zangu wakaja nao wakampa matusi ya kutosha,baada ya siku mbili mzee akaenda kushitaki kituoni kwamba sie ni wezi tukaja kukamatwa usiku mida ya saa nane tukiwa tumelala mlango ukagongwa tulifungua tukafungwa mashati na pingu mikononi mpaka kituo cha polisi mpaka asubuhi,tulikamatwa wanne tena wawili tulikuwa wanafunzi,wengine wawili walikuwa saidia fundi garage, asubuhi ikaja kuripotiwa kwamba watoto wamepotea pale kituoni ikabidi afande aulize "ndio yale majambazi tuliyokamata usiku?"cha kushukuru sura zetu na wizi haziendani maana hata bangi wala pombe hatukuwahi kutumia ikabidi afande aelezwe full story A to Z ndio tukaachiwa tena free bila kutoa hata senti,hiyo ndio ilikuwa siku niliyolala selo japo katika maisha yangu nilishajiwekea siku za nyuma kwamba siwezi lala selo mimi,siwezi kusahau aisee
Ina maana huyo mzee alikuwa anakutongoza ili akufire au ni vipi?
 
Unanikumbushia tar. 22/4 /17 hadi 25/4/17 sikula siku zote hizo na pia sijawahi kupata choo. Nilikuwa na hasira iliyopitiliza
 
2015 niliwekwa ndan polis mwenge pale baada a kituo cha kawe kunipanch kosa nilipiga dreva na konda daladala za Bagamoyo
Ndan ya gari nkakinukisa balahaaa ila niijuta baadaye baada ya maasaa kaa matatu manne tukayanenga na askar na wapigwaj yakaisha nikatoka
 
Ilikua 2014 hv mwshoni, nilikua naenda Shivas na rafiki ang kusafisha macho sasa tumepakia pikpik mishkaki ile tumefika tu paaap tukapigwa pingu pelekwa kwny defender daaah aisee defender sio sehem nzur tulichezea virungu ... Tukapelekwa kituo cha polisi kaloleni bahati nzuri kuna polisi alituonea huruma so tukayajenga tukaachiwa usiku huo huo mida ya saa sita hv tukaona isiwe kesi tukarud shivas tena kuondoa stress mpaka asubh
 
Nilitiwa ndani nikalala kwenye mlango wa chooni pale.... Ila varangati lake mpaka polisi walinifukuza selo wakaniachia.... sipendi ujinga wa kuonewa
 
ippmedia.com/sw/makala/mamlaka-ya-ukamataji
April 17, 2018
Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA YA UKAMATAJI

KWA mujibu wa Sheria Namba 9 ya Mwaka 1985 ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai iliyofanyiwa masahihisho mwaka 2002,...

LmFEpR

Ukamataji ni kitendo cha kumzuia mtu au kumnyima mtu uhuru wake wa kwenda anakotaka, ili afikishwe Kituo cha Polisi kwa ajili ya upelelezi na hatimaye afikishwe mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.

Mtu atahesabika kuwa amezuiliwa ikiwa atakuwa mikononi mwa Afisa wa Polisi, kwa madhumuni yanayohusiana na upelelezi wa Kosa la Jinai na atakuwa chini ya ulinzi kutokana na kosa analotuhumiwa kutenda au kulifanya.

Pia, mtu atahesabiwa kuwa amezuiliwa kihalali au kisheria, iwapo atakuwa ameongozana na afisa wa Polisi au atakuwa na afisa wa Polisi anayesafiri naye katika gari kwa madhumuni ya upelelezi.

Wanajamii wanapaswa kutambua kuwa kuna mamlaka ya kukamata bila hati aliyonayo Polisi, Hakimu na Raia.

Wote hawa wana mamlaka ya kumkamata muhalifu pindi anapofanya au anapotenda kosa mbele yake.

Ifahamike kuwa kila raia pia ana uwezo wa kukamata kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria ya mwenendo ya makosa ya jinai.

Kila raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amepewa uwezo wa kumkamata mtu yeyote ambaye atatenda kosa mbele yake na endapo wakati huo kutakuwa hakuna askari katika eneo hilo.

Pia kifungu cha 31 cha Sheria hii kinaelekeza kwamba; raia yoyote mara baada ya kumkamata mtuhumiwa atamkabidhi kwa Afisa wa Polisi au atamkabidhi kwenye Kituo cha Polisi kilicho karibu naye.

Kama hakuna Kituo cha Polisi kilicho karibu; atamkabidhi mtuhumiwa kwa walinzi wa amani walio karibu yaani Mahakama au Hakimu, Mtendaji wa Kata, Mtendaji wa Kijiji au Mtaa au hata kwa Mwenyekiti wa Mtaa au Kitongoji.

Uhuru huu unaotolewa kwa mujibu wa sheria kwa raia, haupaswi kutumiwa vibaya kwa kujichukulia sheria mkononi au kuchukua nafasi ya mahakama na kutoa hukumu dhidi ya mtuhumiwa kwa kumpiga, kumjeruhi au kumuua. Sheria hii haimruhusu raia yeyote kujichukulia sheria mkononi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa amesema “inashangaza sana pale raia anapopewa mamlaka ya kumkamata muhalifu pindi anapotenda kosa mbele yake na raia huyo kuamua kujichukulia sheria mkononi kwa kuanza kumpiga, kumdhuru na wakati mwingine kumuua mhalifu jambo ambalo ni kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za Ukamataji. Ni marufuku raia yeyote kujichukulia sheria mkononi kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea kujikuta upo mikononi mwa dola.”

Afisa wa Polisi amepewa uwezo wa kukamata bila hati ya kukamatia chini ya kifungu cha 14 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Afisa wa Polisi anao uwezo wa kumkamata mtu endapo mtu yeyote anatenda kosa au kusababisha uvunjifu wa amani mbele yake.

Pia anaweza kumkamata mtu endapo, mtu huyo anajaribu kutoroka kutoka katika ulinzi halali mbele ya Afisa wa Polisi na mtu yeyote ambaye atamzuia Afisa wa Polisi kufanya kazi yake.

Mtu yeyote atakayekutwa katika mazingira yanayoashiria wazi uvunjifu wa amani au katika dhamira ya kutenda kosa au anazurura barabarani kwenye viunga vya bustani za mji nyakati za usiku, mtu yeyote ambaye atakuwa na vyombo vinavyosadikiwa ni vya uvunjaji wa nyumba au atakuwa na silaha za hatari maungoni mwake pia ataweza kukamatwa na Afisa wa Polisi.

Vievile Polisi ana mamlaka ya kumkamata mtu yeyote atakayekutwa na mali au vitu vinavyodhaniwa ni vya wizi au vimepatikana kwa njia isiyo halali na kumkamata mtu yeyote ambaye anaamini kuwa hati ya kukamatwa imetolewa dhidi yake.

Mtu yeyote ambaye Afisa wa Polisi anaamini anakashifu Nembo za Taifa, Fedha au kwa namna yeyote ile inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani na mtu yeyote ambaye anaamini kwa sababu za msingi kuwa ni mzururaji, mbabaishaji na kwamba hana anuani maalum wala shughuli za kujipatia kipato halali.

Hakimu naye ana uwezo wa kukamata kwa mujibu wa Kifungu cha 17 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ambacho kinatamka bayana kuwa hakimu anao uwezo wa kumkamata mtu yoyote anayetenda kosa la jinai mbele yake.

Pia, Hakimu anao uwezo wa kutoa hati ya kumkamata mtu yeyote ambaye ataamini kwa sababu za msingi kuwa ametenda kosa la jinai lakini uwezo huo wa kukamata na kutoa hati ya kumkamata mtu, unaishia kwenye mipaka ya himaya ya mahakama husika.

Imetolewa na

Kitengo cha Uhusiano, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom