Tuliowahi kununua/kupata huduma bila umuhimu wowote, ili mradi unanyemelea mrembo tukutane hapa

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,112
Reaction score
4,361
Habari zenu,
Katika maisha hasa haya ya kusaka warembo wanaume wengi tumejikuta watu wa kufanya mambo bila ridhaaa kupenda.

Mm si mpenz wa kunywa maziwa kabisa, lakin hapa mjini kuna mdada mrembo anauza maziwa ktk jengo letu, sasa nilikuwa namlia timing na njia pekeee ni ya kunywa maziwa ambayo anayouza, najikuta nayazoea maziwa kwa lazima aiseee, week ya pili sasa nakunywa maziwa yake.

Muda mwingine nawahi kunywa chai yangu ya rangi lakini akifika yeye najikuta naagizia tena maziwa.

Tuliokumbwa na kadhia hii tukutane hapa
 
au ile utakuta umemuona dada ameenda sehemu ambayo hata hukuwa na ratiba nayo au kama yupo shop na wewe unajipeleka unanunua kitu ambacho hata hukutegemea,lkn unamfuata eti kisa tu uanzishe mazoea,mwisho wa siku unachezea kitasa...hawa viumbe hawa.
 
kuna duka nilikuwa naenda kunywa juice kila siku kama mtoto.hii kitu tamu mpaka tunakuwa wajinga.kasichana kalikuwa kazuri sana
 
Kuna njemba hapa street zilikuwa zinakula mapera balaa kisa demu anauza habari walikuwa wanaipata kwenye kutoa haja kubwa. Ila hakuna aliyekula mzigo waliambulia kutatuliwa malinda kila siku na mbegu za mapera.
 
Kuna njemba hapa street zilikuwa zinakula mapera balaa kisa demu anauza habari walikuwa wanaipata kwenye kutoa haja kubwa. Ila hakuna aliyekula mzigo waliambulia kutatuliwa malinda kila siku na mbegu za mapera.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…