Tuliowahi kununua/kupata huduma bila umuhimu wowote, ili mradi unanyemelea mrembo tukutane hapa

Kuna bosi wangu alikua anamtaka demu flani muhudumu wa mgahawa basi daily ilikua lazima atupeleke lunch kwenye huo mgahawa na kutulipia wote tena kwa mbwembwe za kibosi, siku moja usiku akamuona yule demu anaingia room yangu basi tokea siku ile offer ya lunch ikafa na alininunia mbaya tukawa hatuongei huko field hadi tunarudi dar na tulipofika ofisini alinichomesha ile mbaya kisa k.
 
Hivi nyinyi vijana mnapata wapi haya mawazo??

Nimekumbuka miaka ya nyuma kidogoo mwishoni mwa miaka ya 90 hivi, nilijikuta napenda kuingia mskitini huku mimi ni mkristo
Kilichonikuta nikashtukia naletewa kadi ya mchango wa harusi aseeee


Hivi viumbe vina mengi ya kujibu siku za mwisho aseee
 
Nilijiunga Forever kwa ajili ya mrembo aliyekuwa ananisaundisha nijiunge... Nikajiunga kwa ajili yake na niliunguza karibu laki saba kununua 'package' ya kujiunga, bidhaa ambazo 'ziliozea' stoo kwa kuwa sikuwa na mpango na hiyo biashara ya Alovera.
 
Nililundika DAWA ndani boksi zima kisa muuza pharmacy mrembo duka la chuo kila siku lazima nikanunue dawa[emoji26] [emoji26] [emoji26]
 
Yaaaan brother acha tu, nakwambia hapa nakunywa maziwa kila siku, mbaya zaid hata chenji nasamehe kabisa,
 
Nilijiunga Forever kwa ajili ya mrembo aliyekuwa ananisaundisha nijiunge... Nikajiunga kwa ajili yake na niliunguza karibu laki saba kununua 'package' ya kujiunga, bidhaa ambazo 'ziliozea' stoo kwa kuwa sikuwa na mpango na hiyo biashara ya Alovera.
Ulikula mzigo?
 
Nilipitiliza kituo zaidi ya kilomita 60 ili nimsaundishe mtoto niliyekaa naye, nikaruka sarakasi zangu nikaambulia namba ya simu na ahadi kuwa lazima tutaonana.

Tulishuka wote ila yeye alifatwa na bodaboda, mimi usiku ushafika nikazama lodge, mid night nikatumiwa text ya usiku mwema.

Asubuhi nimetoka room sura ya kwanza kuonana nayo koridoni ni yule manzi kumbe alilala next door. Kabla sijamaliza kushangaa likatoka linjemba limejifunga shuka kiunoni, lina afya mara mbili zaidi yangu lina manyoya kifuani kama ngedere. Limeenda kubembeleza mhudumu awape chai mbili kwa kelele sana.

Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kujiona bonge la pimbi na kugeuza nilikotoka. Hata kichai chao cha bure nikasusa.
 
Nikipitiliza mpk dukani cha ajabu kumi kipande sina, dadeki nkavunga naulizia Kemikola! Mangi gani wa Leo atakuwa nazo hizo kemikola bidhaa za zamani hizoooo! Shikamoo mwanamke
 
Kuna njemba hapa street zilikuwa zinakula mapera balaa kisa demu anauza habari walikuwa wanaipata kwenye kutoa haja kubwa. Ila hakuna aliyekula mzigo waliambulia kutatuliwa malinda kila siku na mbegu za mapera.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Yaaaan brother acha tu, nakwambia hapa nakunywa maziwa kila siku, mbaya zaid hata chenji nasamehe kabisa,
Ujue alisha kusoma
Amekaa tayari na shambulizi lako mtongozo wa nguvu.
Ukishindwa au akikata tamaa atakukomvati na kuwa rafiki.
Ataanza kukwambia kuwa anampenda furani tofauti na wewe lakoni mtu huyo anamtesa.
Mwisho wa siku utafaiti kulipinga hilo ili wewe uichukue nafasi.
Atakwambia umechelewa na wewe ni kaka yake,.



Baaaaaaaadae kabisa unakabidhiwa kadi ya mwaliko kwani ya mchango wewe umeshahesabiwa kama kaka yake.


Hapo ndio utajua kabisaa chenji yako imelipia kadi ya mchango[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…