Nilipitiliza kituo zaidi ya kilomita 60 ili nimsaundishe mtoto niliyekaa naye, nikaruka sarakasi zangu nikaambulia namba ya simu na ahadi kuwa lazima tutaonana.
Tulishuka wote ila yeye alifatwa na bodaboda, mimi usiku ushafika nikazama lodge, mid night nikatumiwa text ya usiku mwema.
Asubuhi nimetoka room sura ya kwanza kuonana nayo koridoni ni yule manzi kumbe alilala next door. Kabla sijamaliza kushangaa likatoka linjemba limejifunga shuka kiunoni, lina afya mara mbili zaidi yangu lina manyoya kifuani kama ngedere. Limeenda kubembeleza mhudumu awape chai mbili kwa kelele sana.
Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kujiona bonge la pimbi na kugeuza nilikotoka. Hata kichai chao cha bure nikasusa.