Tuliowahi Kupata Ajali Na Kupona Tukutane Hapa! Tumshukuru Mungu Na Kutoa Somo.

aisee mnaleta utani wadau mimi mwaka jana mwezi wa tatu nilidondoka toka ghorofa ya tatu hadi chini halafu sijavunjika hata kidole, ila nilizimika nilistuka nipo amana napata huduma, shout out kwa dr frank wa amana
Kijana pole sana, dr frank asije akawa kijana mmoja hivi mshkaji wangu?
 
Nilishawai mwagikiwa na mafuta ya kula ya moto yalikua yana kaangiwa kuku wa sherehe, aisee cha ajabu sikuskia maumivu ata kidogo wala sikuungua,
 
Jamaa yuko fresh sana, pole kijana.. Kutoka gorofa ya tatu sio utani mkuu. mungu anakupenda sana
watu hawaamini mkuu maana hata kidole hakikuvunjika, nimeacha kuwashuhudia watu siku hizi maana wanaona kama nawadanganya
 
Ajali ya kwanza mwaka 1997 tukitoka Singida kwa njia ya usandawe kufika sehemu nisiyoijua SAA tatu usiku gari likaanguka niliumia mguu kidogo baada ya mwaka nikagundulika S1 hadi S6 zina matatizo, yapili 2006 Tabata hiyo ndio ilikuwa mbaya sana driver alikuwa mwendo kasi akatuangusha mtaroni nilizimia baada ya kuzinduka tukapelekwa Amana Mimi nikaomba nipelekwe Hindu Mandal kule wakanikataa wakasema hii ni kesi kubwa nipelekwe Muhimbili ambapo nilipata matibabu na kupona ya tatu natoka Mwanza Dar kufika pandambili tukapata ajali ikabidi tulale porini maana driver aliliingiza porini kuokoa maisha yetu ni hadithi ndefu ila nashukuru Mungu ni mkubwa zote hapo tuliumia lakini hakuna aliyepoteza maisha, kwa kweli ajali muisikie tu
 
Nakumbuka nikiwa mdogo darasa la kwanza mida ya sa4 nikienda zangu shule gari likawa linakuja nyuma taratibu m niko mbele nikapisha pembeni kabisa yule jamaa akanifata mpaka nje ya barabara alikua bishoo mmoja aliazima gari kwa ajili ya misele na nilichogundua jamaa alikua ame concentrate kumcheki dada mmoja anaitwa Eve (mashallah) jirani yng.

Jamaa kutahamaki anakaribia kunigonga m fasta nikaruka mtaro jamaa akashindwa kuControl akaingia mtaroni gari likabinuka nilikua mdogo hilo tukio sijasahau mpaka leo and i always say there is God above..
Mchizi alitoka salama bad thing msala woote akanisingizia mimi kuwa ndio source namm kama mtt nilishindwa kuongea ila nilijua source ilikua ni yy.
 
sitosahau ajali niliyopata unguja maeneo ya bwawani hoteli.Dereva (Jecha) pale alipogeuza gari juu chini chini juu niliumia sana.ajali isikie tu
 
Namshukuru sana Mungu tena nilichogundua watu wanajifanya hakuna Mungu kwenye ajali kila mtu anatambua uwepo wa Mungu na kumuomba msaada
 
Ajali nyingine m na wanangu tulifakamia mti wa mpera tukajazana juu kama 10 hiv kumbe mti umeoza chini kilichotokea sasa, mti ukaanguka tuko juu" washaji zangu waliumia sanaa ila mm sikutoka hata na mchubuko"
 
Pole sana my friend
 
Mimi sijawahi pata ajali lkn nimesha shuhudia nyingi sana.

Moja ninayoikumbuka ni ya jamaa mmoja mlevi alikufa kwa kuungua na moto wa sigara, uliunguza godoro pamoja na yeye mwenyewe.

Nakumbuka jamaa alikua cha tonji mbaya.

Siku hiyo karudi kalewa, kapanda kitandani kwake, kbla haja lala, akalipua sigara yake ili imbembeleze kumbe ndio inakua chanzo cha kifo chake.

Baada ya kuvuta sigara yake akatupa kipisi kilicho baki, amadi, kumbe kipisi hakikuanguka chini, badala yake kikaangukia kwenye godoro.

Bila ya ufaham na uchovu wa pombe kipisi kiliunguza godoro lote na kumkusanya na yy mwenyewe.

Nakumbuka kati ya majirani wa kwanza kuingia chumbani na mm nilikuwepo, nilimshuudilia Njata bomba ukiwa ndio anamalizikia kupasuka Kichwa.
Asikuambie mtu kichwa kinabutuka utadhani bomu.

Zilipita siku mbili bila kuhisi ham ya kula.

HIYO NDIO AJALI NINAYO IKUMBUKA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…