Mimi sijawahi pata ajali lkn nimesha shuhudia nyingi sana.
Moja ninayoikumbuka ni ya jamaa mmoja mlevi alikufa kwa kuungua na moto wa sigara, uliunguza godoro pamoja na yeye mwenyewe.
Nakumbuka jamaa alikua cha tonji mbaya.
Siku hiyo karudi kalewa, kapanda kitandani kwake, kbla haja lala, akalipua sigara yake ili imbembeleze kumbe ndio inakua chanzo cha kifo chake.
Baada ya kuvuta sigara yake akatupa kipisi kilicho baki, amadi, kumbe kipisi hakikuanguka chini, badala yake kikaangukia kwenye godoro.
Bila ya ufaham na uchovu wa pombe kipisi kiliunguza godoro lote na kumkusanya na yy mwenyewe.
Nakumbuka kati ya majirani wa kwanza kuingia chumbani na mm nilikuwepo, nilimshuudilia Njata bomba ukiwa ndio anamalizikia kupasuka Kichwa.
Asikuambie mtu kichwa kinabutuka utadhani bomu.
Zilipita siku mbili bila kuhisi ham ya kula.
HIYO NDIO AJALI NINAYO IKUMBUKA.