Tuliowahi Kupata Ajali Na Kupona Tukutane Hapa! Tumshukuru Mungu Na Kutoa Somo.

Tuliowahi Kupata Ajali Na Kupona Tukutane Hapa! Tumshukuru Mungu Na Kutoa Somo.

Nakumbuka nilikuwa nimempakia babu yangu maeneo ya morogoro kwenye baiskeli,sas ile njia siiikumbuki,ila babu km sehemu mbaya ananiambia kwamba tushuke,maaana njia ilikuwa na kona nyingi mno,almost njia yote ikuwa ya kona,sas kumbe babu amelala mm nikiwanasikilizia director wangu,sasa ile nakata kona babu ndio kastuka maaana alikuwa anasinzia,akaniambia pabaya tushuke,aaaakha wapi baiskeli imechanganya ile speed kufunga brake zote zilikatika,nakumbuka baabu alianza kulia,sasa kitu kimewiva hatari huku mzeee analalamika endapo tukifika chini tutapasuka vibaya nadhani hata kufa pia,kwan pembezoni kulikuwa na mawe makubwa sana na mengi,lakini mchezo nilioucheza we acha tu"NAMUOMBEA KWA MUNGU APUMZIKE MAHALI PEMA BABU YANGU KIPENZI"
 
Ajali nyingine m na wanangu tulifakamia mti wa mpera tukajazana juu kama 10 hiv kumbe mti umeoza chini kilichotokea sasa, mti ukaanguka tuko juu" washaji zangu waliumia sanaa ila mm sikutoka hata na mchubuko"
Umenikumbusha kitu hapa.
 
Mm nakumbuka ya ndege mwaka 2010,yaaan ndege ilivyofika angani badala ya kwenda mbele ikawa inarudi nyama,basi rubani akaona sio shida akaiyacha tukarudi nyuma ilivyotaka yenyewe ikatua kwenye mashamba ya tumbaku Zimbabwe
bangi mbaya sana
 
Nakumbuka nilikuwa nimempakia babu yangu maeneo ya morogoro kwenye baiskeli,sas ile njia siiikumbuki,ila babu km sehemu mbaya ananiambia kwamba tushuke,maaana njia ilikuwa na kona nyingi mno,almost njia yote ikuwa ya kona,sas kumbe babu amelala mm nikiwanasikilizia director wangu,sasa ile nakata kona babu ndio kastuka maaana alikuwa anasinzia,akaniambia pabaya tushuke,aaaakha wapi baiskeli imechanganya ile speed kufunga brake zote zilikatika,nakumbuka baabu alianza kulia,sasa kitu kimewiva hatari huku mzeee analalamika endapo tukifika chini tutapasuka vibaya nadhani hata kufa pia,kwan pembezoni kulikuwa na mawe makubwa sana na mengi,lakini mchezo nilioucheza we acha tu"NAMUOMBEA KWA MUNGU APUMZIKE MAHALI PEMA BABU YANGU KIPENZI"
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Majanga hayo yashawah kukukuta nini na wewe?
Ndio. Nakumbuka tulienda beach na washikaji. Sasa tukaenda kwenye mikoko. Tukapanda kwenye mti watu kama sita hivi tupo kwenye tawi moja tukaanza kusikia kitu kama kinavunjika kumbe ndo hilo tawi tulilokalia mara wote chini liwe tawi likaja kutufunika. Tulishukuru chini kulikuwa mchanga sababu tulikuwa beach
 
Mm nakumbuka ya ndege mwaka 2010,yaaan ndege ilivyofika angani badala ya kwenda mbele ikawa inarudi nyama,basi rubani akaona sio shida akaiyacha tukarudi nyuma ilivyotaka yenyewe ikatua kwenye mashamba ya tumbaku Zimbabwe
Acheni kuharibu thread za wenzenu
 
Aiseeee hakuna mtu alikuaga bure kabisa kama mimi wakati nakua ila yaliponikuta siitamani hata ajali ya kujikwaa......
Ilikua 2001 kipindi hicho nipo darasa la tano....nakumbuka mwaka huo tulihama kutoka obay tulipokua tunaishi tukahamia tegeta kwenye makazi yetu rasmi. Kwa hiyo nilikua natoka zangu tegeta to obay kila siku kwenda shule.
Sasa shida ilianzia kwenye kusave nauli kisa kununua sun vita za ziada....nilikua mi na my bro tulikua tunapewa nauli mia mbili(enzi hizo nauli 50 tu.....daah maisha kweli yako speed) na miambili nyingine ya kutumia kila mmoja. Hapo tulikua tunapanda basi tegeta mpk mwenge thn mwenge to mbuyuni halafu pale tunatembea mpk obay p/school.
Sasa tukajikuta wajanja instead ya kupanda basi hivyo tukaanza kupanda gari za tegeta k/koo enzi hizo ni dcm tu na lazima zipitie kwanza bahari beach ndo ziende k/koo. Kwa hiyo tukipanda hizo dcm tulikua tunashuka zetu morroco, pale tunakutana na washikaji zetu wa kinondoni tunaanzisha mdogo mdogo mpk shule. Hapo tunakua tumesave mia kwenda na kurudi.

Sasa ujinga wangu ulikua huu.
Tukipanda zile dcm konda alikua ananiambia nipite mbele kabisa kwa dereva, nikawa nakaa pale kwenye engine. Sasa nikiwa pale mbele zile gari zilivyokua zinapishana nikawa najiwazia moyo "natamani hizi gari zikutane uso kwa uso nione itakuaje" yani hiyo ndio ilikuaga sala yangu kila siku nikikaa pale mbele.

Mungu ajibu maombi
Siwezi isahau hiyo siku asubuhi tumetoka zetu home mimi bro kama kawaida yetu tukadaka dcm letu mpk morocco tukakutana mshikaji wetu mmoja tukaanza mdogo mdogo....kabla hatujafika osterbay police hapa juu kidogo, si tukasikia kengere ya baiskeli inagongwa nyuma yetu, wenzangu wawili wakapisha kulia na mimi nikapisha kushoto. Daaah huezi amini yule jamaa nae baada ya kupita pale kati tulikompisha si akanifata mimi nilipo. Aiseee alinivamia yule jamaa na phoenix yake na ukizingatia kile kibarabara ni cha lami na kina kama kimteremko fulani hivi, basi nilibimbilika pale chini sisahau. Mpaka leo nina kovu mkono wa kushoto na magoti yote mawili na toka siku hiyo nilikoma kuomba gari zigongane nikajisemea kama baiskeli tu vile gari je itakuaje?

Daah ilikua issue sana kwa b.mkubwa alipokuja kuona eneo la ajali, swali likarudi kwetu na miplasta yangu pale mlifikaje mpk ugongwe? Ilibidi kueleza kila kitu. Mpk napona sikurudi tena obay b.mkubwa aliona ujinga akatuamisha.
 
Mm nakumbuka ya ndege mwaka 2010,yaaan ndege ilivyofika angani badala ya kwenda mbele ikawa inarudi nyama,basi rubani akaona sio shida akaiyacha tukarudi nyuma ilivyotaka yenyewe ikatua kwenye mashamba ya tumbaku Zimbabwe
Mkuu acha kudanganya watu . Ndege ikawa angani haiwezi kurudi nyumba. Ni mbele, kulia ,kushoto unless you're doing aerobatic ndipo unaweza ku spin na vitu kama hivyo lakini ndege hairudi nyuma ikiwa angani .
 
Nakumbuka kuna siku wakati natembea Tabata relini sijui hili wala lile kumbe kuna lori limehama njia basi natembea tu kitozi.....Ebwana kuja kushtuka nakuta tairi mguuni kwangu baada ya lori kuingia mtaroni.....

Nyingine kuna siku nikiwa Dogo nilienda kuogelea Coco beach si nikajifanya fundi nilizama na kunywa vikombe vya haja ht csijui washikaji waliniokoaje, Nilitoa macho km chura...hadi leo hata nishikiwe fimbo sitaki kuogelea staili yangu ni kuingiza miguu tu

SITASAHAU

hahahahahaha! mkuu hiyo style ya kuingiza mguu tu! matata sana
 
Mm nakumbuka ya ndege mwaka 2010,yaaan ndege ilivyofika angani badala ya kwenda mbele ikawa inarudi nyama,basi rubani akaona sio shida akaiyacha tukarudi nyuma ilivyotaka yenyewe ikatua kwenye mashamba ya tumbaku Zimbabwe
Mmh!
 
Nakumbuka kuna siku wakati natembea Tabata relini sijui hili wala lile kumbe kuna lori limehama njia basi natembea tu kitozi.....Ebwana kuja kushtuka nakuta tairi mguuni kwangu baada ya lori kuingia mtaroni.....

Nyingine kuna siku nikiwa Dogo nilienda kuogelea Coco beach si nikajifanya fundi nilizama na kunywa vikombe vya haja ht csijui washikaji waliniokoaje, Nilitoa macho km chura...hadi leo hata nishikiwe fimbo sitaki kuogelea staili yangu ni kuingiza miguu tu

SITASAHAU
alaa! kumbe na ubitoz wote huo kuogelea nehi!?
 
Back
Top Bottom