Tuliowahi kupata division zero na four tukutane hapa. Je, tunajuta?

Tuliowahi kupata division zero na four tukutane hapa. Je, tunajuta?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Wazee wa baka bencha mpo (ilininichukua miaka mingi kujua kwamba Ilikua inamaanisha back bench yaani seat ya nyuma 😁😁).

Nimeingia secondary Mwanza pale nyakabungo nikazingua vibaya mno nikafukuzwa Shule nikahamia Thaqafa secondary kwa ogweyo na opiyo nikatandika zero takatifu.

Screenshot_20230223-095711~2.png


Kiukweli nilizingua sana sikuwahi kupenda kusoma kabisa, ukorofi Mimi, mipira Mimi, utoro ndio Ilikua jadi yangu, Mibangi sana naenda Shule saa 2 saa 5 nimepotea (nyakabungo Hapo).....

Thaqafa pale nimeruka ukuta kwenda kuzurura town (nilipelekwa boarding na mzee) niliona Shule kama mateso tu, Mwisho wa siku nikapata division zero nzuri tu.

Nimekuwa baba Sasa kiukweli siwezi kumdanganya mtoto wangu kwamba nilikua na akili saaana (kama wazazi mnavyowadanganya watoto wenu) Ila vice versa mtoto wangu Yuko la kwanza naona kama anajitahidi sio kama Mimi baba ake labda karithi akili kutoka kwa mama ake.

Navyoyaona maisha kwa Sasa, Kuna watu wamezaliwa ni given wako na uwezo tu msuli kidogo matokeo makubwa, wapo ambao walikua na msuli temboo matokeo sisimizi kama ya kwangu tu.

Nimezaliwa kwenye familia ambayo wengine walipata division one Lakini Mimi nilipata zero je Mimi ni kilaza? 😁😁 Au sikua serious?

MTAZAMO WANGU
Elimu ni nzuri sana, ukitaka kua na pesa kwenye elimu basi inabidi usome saaana kwa viwango vya juu basi Hapo utamiliki pesa, pasipo elimu Kuna viwango ambavyo uwezi kuzifikia.

Baada ya kupata zero mzee wangu alinambia neno moja, POPOTE PALE ULIPO KATIKA ENEO ULIPO UFANYE KAZI KWA JUHUDI NA BIDII SAAANA, Uwe umesoma au hujasoma juhudi na bidii nadhani ndio ufunguo wa kutengeneza milo mitatu kwa siku, hii ndio principle ninayotembea nayo huku mashambani.

Wenzangu tuliopata zero je tunajuta? Je, unatamani kurudi shule kusawazisha makosa? Mtoto wako akipata zero utaumia?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Maisha yangu ya shule toka naanza hadi mwisho napata one tu, chuo ndio kidogo niliyumba ila mtaani sasa napata division zero saana wakati wale wa zero wanang'ata pera mbele huko.

Kuna mwamba alikuwa mtoro balaa, mlevi, anafeli vibaya mno sahizi yupo itali kaoa mzungu na anapiga biashara. Sahizi anatushauri yy kuhusu maisha.
 
Mimi bhana darasa la tatu mpaka la saba sikuwahi kutoka nje ya namba 1-3

Secondary nikawakimbiza shule ya Kata mock zote Na necta ni one Na two division

Advance nikazingua PCB ila nikaenda chuo Fulani nikabutua GPA YA KAWAIDA UPPER SECOND ILA KWENYE INTERVIEW YAO UTUMISHI SIKUFANYA MAKOSA NIKAONYESHA UWEZO WANGU KWELI NIKABUTUA NIKAJA KAZINI NIKAONYESHA TENA UWEZO WA KAZI nikakubalika sana na maboss kwenye utendaji LICHA YA MADHAIFU YANGU NA HASA MITUNGI..

NIKAJA KWENYe KUCHAGUA mke kweli sijakosea NIKAJA kwenye kujaza mimba sijafanya kosa ni kubutua tu..NIKAJA kwenye ujasiriamali Na biashara hapa bado napambana ila Nina bonge la idea kila siku linaniingizia 8500 nimekaa tu....
 
Back
Top Bottom