Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Sasa elfu 50 ndio unatoa wengi? Hauko serious
 
Mara nyingi pesa huwakuta watu wajinga na wasio na mipangilio..
 
Kupata milioni nne point something na kisha zikaisha ndio kupata hela nyingi na kufilisika? Nilijua ulikuwa level za kina Bakhresa au Ginimbi.
Hata mimi nawashangaa wengine wanasimulia hadi million za madanga ,khaa.

Bora hata min.iwe 10mln ,chini ya hapo ni pesa za kuhonga na hazifilisi mtu.
 
Huu uzi unafurahisha na kufunza [emoji23][emoji23]nitarudi tena kupitia comments zikishaongezeka

Jimena
 
Haahahah
 
Natamani kuijua hiiyo biashara....
 
Japo kuwa humu zingine zina chumvi ila nimejifunza

2019 nikiwa sina lile wala hili kuna jamaa yangu akaniambia twende tukazamie migodi wapi hiyo Msumbiji basi tumefika kule tukapata kisehem tukapiga kama Zari hivi tukapata mzigo kwenda kupiga bei
Umetema kama m630 ukija kupiga pasu mtu mbili kama m300

Tokea hapo tukakataana urafiki kila mtu aliingia njia zake mana jamaa yangu akadai tukawekeze mim nikaona kuzeeshana mapema huku mi nikaenda zangu dar bila kupitia hom

Fika dar mkwanja si upo kwa bank nikakodi gest nzima nikatafuta mabamnsa kwaajili ya ulinzi tafuta pisi kali kama 10 hivi wakiwemo na mastaa wakike watatu nilikaanao pale gest kwa siku 10 na kubakiwa na laki mbili ya nauli ya kurudi hom mbeya fika hom nikala msoto wa ajabu haijawahi tokea toka nije duniani toka anga za mbali mwaka ukapita nakutana na jamaa yangu ana kampuni yake songea ya usafirishaji mizigo scania kama 23 kumbe mwenzangu aliwekeza kule kele kwenye migodi

Sio siri maumivu yalizidi kusikia hivyo nikamwomba anipe nafasi ya udereva kwenye kampuni yake mana nilikuwa nimepitia huko kabla
Kwakuwa tulikuwa kama ndugu

Akaniambia hapana siwezi kukupa nafasi tena asee kusikia hvy maumivu yalizidi nikajiona sifai nimetengwa na dunia baada ya hisia kunishinda nikatafuta sumu ya panya nikaenda mbali kdg na hom nikanywa
Imepita dakika mbili mwili ukaanza kunyong'onyea macho yanaanza poteza nuru machozi yakinilenga nikikumbuka yote niliyoyafanya ,
Nikasema Mungu naomba unisamehe kwa yote niliyokufanyia ambayo hayakukupendeza

Punde si punde nikiwa kwenye hali hiyo akatokea jamaa yupo na kipkpk akawa anasikia kama kilio hivi cha kugurumia sikujua kilichoendelea ila nilijikuta hospitali nimewekewa ma dripu tazama pembeni jamaa yangu yule wa migodi nimekaa hospitali siku sita

Nilivyokuwa fresh jamaa akaniambia sasa nazani umepata funzo kwenye maisha yako akaacha hom m2 kwaajili ya matumizi akanichukua tukaenda migodi akanipa eneo na kuniambia pambana

Nikatafuta nyoka yaani wafanyakazi lugha za migodi hizo, tukapiga kazi Mungu si asumani nikapata jiwe la pesa ndefu nakumbuka waliungana kama wanunuzi wa madini watatu kuuchukua ule mzigo nikawapa wale nyoka m200 kila mmoja, walikuwa nne nikaenda kwa jamaa akanipa somo jinsi ya kukaa na hela isipukutike hovyo bila kukusudia nakumbuka pesa yote aliniachia ninapo sema pesa ni pesa kweli

Akaniagizia kama Volvo za mizigo 14 hivi za kichina akawa anazisimamia yeye si unajua watu wa nchi hiyi wakijua unapesa ukikoswa na majambazi basi yatakukuta yale ya jamaa wa mtwara na polisi alijinyonga kwa taulo nchi hiyi ni mwiko kuwa na pesa za ghafla basi nikajenga ka nyumba kakisasa kwajili ya wazazi, fungua pub ya nguvu mbinga na dar anzisha kiwanda kidogo cha unga songea hayo yote nimefanya kwa mgongo wa jamaa sikutaka nijulikane kama nina pesa alafu nikamwambia nipe kazi kwenye hiyo kampuni yako nikawa kama dereva mtiifu baada ya wiki tunakutana kwa siri kujadili hali ya uchumi wetu na mpaka sasa hakuna anayejua mm nina shera kwenye kampuni ya jamaa zaidi ya family yangu maisha yangu ya kawaida sana na hata kwenda kwa miguu kazini kawaida kukaa kijiweni kucheza bao draft kawaida yote haya nimejifunza niliyopitia jamaa wanajua mm ni mwajiriwa wa rafiki yake na kuongea ooh alipata hela kachezea mpaka akanywa sumu ila hawajui kinachoendelea sina cha kupoteza ila nimejifunza sio hayo tu kuna mengi ndani yake ambayo ukifuatilia nyuz zangu utawapata japo nilididimia hapa katikati ila nimekaa sawa

Nb kufilisika sio mwisho changa upya karata zako yote yanawezekana mwanaume pambana kisawasawa acha kulia lia sijui ndio basi kazaaaa kubali kufa ukipambana acha kuwaza waza pambana mpaka uache alama kwenye dunia ameen

Na huu ndio ukumbusho wa picha kati ya pesa ambazo tulikuwa tukigawana hukoo machimbo enzi hizoo nikiwa kwa digar na jamaa zangu[emoji116][emoji116]2020View attachment 2098320
 
Braza c chai kweli
 
Braza c chai kweli
Hapo sasa inategemea na unavyoamini ww msomaji akili itavyokwambia ni hvy hvy ila ukweli wa mambo ninaujua mm mwenyewe nikiwa hapa mgahawa mchana huu nikipata ugali maharagwe na kisamvu bila kusahau kitimoto robo kilo japo cha leo mifupa kikubwa tutafute pesa na pesa haijawahi tosha ukiona umetosheka pesa jua ndio dalili za kuanza kufilisika aya mengine niachie mwenyewe View attachment 2098309
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…