Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Mimi kanuni yangu ,nikipata hela nyingi ,natenga kiasi cha kutolea wenge na kingine naficha kabisa,nikiangalia jinisi nilivokitumia ,roho ikiuma basi sigusi zilizobaki.

Mfano nimepata mil 1 za ghafla ,elf 50 natolea wenge.

Hela za ghafla ambazo kukutegemea au hujawai shika ,zinaweza kufanya ukawa mjinga au broke kuliko ulivo sasa.

#tujiandae kisaikolojia ,kwamba ,matumizi mabovu nisawa na tundu dogo chini ya tanki LA maji ,linavujiasha polepole Ila linawez maliza maji lisipozibwa

$kuna upande wa Bahati mbaya ,mazingira ya kazi au biashara ,ni kusali sana na kuchukua tahadhari na kushirikisha washauri wa masuala ya fedha na familia
Sasa elfu 50 ndio unatoa wengi? Hauko serious
 
🤣🤣🤣 hufai kufarijiwa kbs aisee...hv mnazuzuka nn kuhonga gari??yaan bora ungemfungulia biashara ila iwe yako lakini usimamiz na ww unakuwepo..akizengua unamfukuza mapemaaa!mtu wa kumnunulia gari ni wife tu!..ww hufai ht kubenbelezwa jibembeleze mwenyewe
Mara nyingi pesa huwakuta watu wajinga na wasio na mipangilio..
 
Kupata milioni nne point something na kisha zikaisha ndio kupata hela nyingi na kufilisika? Nilijua ulikuwa level za kina Bakhresa au Ginimbi.
Hata mimi nawashangaa wengine wanasimulia hadi million za madanga ,khaa.

Bora hata min.iwe 10mln ,chini ya hapo ni pesa za kuhonga na hazifilisi mtu.
 
Huu uzi unafurahisha na kufunza [emoji23][emoji23]nitarudi tena kupitia comments zikishaongezeka

Jimena
 
Mwaka 2012/2013 tulipiga 50M, mimi na msela wangu kwenye company moja ya vinjwaji huko Kanda ya Ziwa! Tukagawana 25M!

Ilikua Ijumaa,nikakata fast jet,faster Dsm,saa kumi na moja tukasepa Mwanza,bondeni hotel pale magomeni ndiyo nikawa nalala pale! Baada ya kufika dsm saa moja hivi za jioni,mwanangu mmoja alikua Sinza Mgabe pale,fanya Mpango Shangazi Ezekiel alichezea koki kwa siku hiyo,hadi asubuhi kwa laki tano,hapo toa gharama ya vinjwaji na chakula plus ticket ya ndege,chumba cha kulala,maana yake 2M inakata hiyo, Basi bwana,kesho yake nikashinda nimelala tu, kozi ya uchovu na Pombe na gegedo! Usiku tukazama Casino pale Palm Beach,tukapigwa laki 5,tukaenda the Grande tukapigwa laki 5,basi hapo Mimi nasema haina shida pesa ipo! Tukaenda The Princess pale IT Plaza,aiseee tukapiga 5M! Jamaa akasema tusepe,hapo nishalewa,kulikua na demu flan hivi Mfilipino,alikua anauza nikasema twende,bei USD 500! Nika change pale pesa,nikawa na USD kama 100 hivi! Jamaa yangu akasepa zake,kaniacha,nikachukua yule demu,nikaenda kula!

Kesho yake nikarudi pekee yangu Casino,si wakanila 3M! Nikaondoka kurudi Hotel,hapo kwenye 25M bado kama 20M hivi!

Nikarudi Mwanza,fanya fujo sana,nikaja shituka nina 10M! Nikanunua kiwanja na furniture za ndani pesa yote kwisha! Nikasema sasa hapa tupige deal tena nianze kujenga,deal likawa dirisha,kikaota,nikasepa zangu shytown! Hangaika sana ramani hazisomi! Ikabidi niende tu kwenye company za wavaa overall! Maisha na pesa ni kama shetani hivi hua anakuja!

Sent using Jamii Forums mobile app
Haahahah
 
Nilifurukuta kwenye mvua na jua, usiku na mchana kwenye kazi za kutumwa, zenye maudhi ya kila aina, dhulma na visasi nikafanikiwa kupata mtaji kama m7, mzee baba nakomaa nayo hiyo kidogo sasa ka business kamefikia mtaji wa m15 ndani ya mwaka mzima, alafu biashara moja ya kidwanzi machoni pa watu lakini mm kwangu ni tamu kama nguruka, najenga ka mjenho ka pili, kupitia hiyo hiyo biashara bila ya kuingilia mtaji

Huko nyuma nishawahi kumiliki b2 ( ki ukweli nazo nilizipata kimazabe na zikaisha kimazabe ) nilichofanyia mpaka sasa sijui *****, lakini kufupisha tu story nilikutana na wacongo na waganda hawa watu sio poa, walinifanya niongee pekeyangu kwa miaka kadhaa.
Natamani kuijua hiiyo biashara....
 
Japo kuwa humu zingine zina chumvi ila nimejifunza

2019 nikiwa sina lile wala hili kuna jamaa yangu akaniambia twende tukazamie migodi wapi hiyo Msumbiji basi tumefika kule tukapata kisehem tukapiga kama Zari hivi tukapata mzigo kwenda kupiga bei
Umetema kama m630 ukija kupiga pasu mtu mbili kama m300

Tokea hapo tukakataana urafiki kila mtu aliingia njia zake mana jamaa yangu akadai tukawekeze mim nikaona kuzeeshana mapema huku mi nikaenda zangu dar bila kupitia hom

Fika dar mkwanja si upo kwa bank nikakodi gest nzima nikatafuta mabamnsa kwaajili ya ulinzi tafuta pisi kali kama 10 hivi wakiwemo na mastaa wakike watatu nilikaanao pale gest kwa siku 10 na kubakiwa na laki mbili ya nauli ya kurudi hom mbeya fika hom nikala msoto wa ajabu haijawahi tokea toka nije duniani toka anga za mbali mwaka ukapita nakutana na jamaa yangu ana kampuni yake songea ya usafirishaji mizigo scania kama 23 kumbe mwenzangu aliwekeza kule kele kwenye migodi

Sio siri maumivu yalizidi kusikia hivyo nikamwomba anipe nafasi ya udereva kwenye kampuni yake mana nilikuwa nimepitia huko kabla
Kwakuwa tulikuwa kama ndugu

Akaniambia hapana siwezi kukupa nafasi tena asee kusikia hvy maumivu yalizidi nikajiona sifai nimetengwa na dunia baada ya hisia kunishinda nikatafuta sumu ya panya nikaenda mbali kdg na hom nikanywa
Imepita dakika mbili mwili ukaanza kunyong'onyea macho yanaanza poteza nuru machozi yakinilenga nikikumbuka yote niliyoyafanya ,
Nikasema Mungu naomba unisamehe kwa yote niliyokufanyia ambayo hayakukupendeza

Punde si punde nikiwa kwenye hali hiyo akatokea jamaa yupo na kipkpk akawa anasikia kama kilio hivi cha kugurumia sikujua kilichoendelea ila nilijikuta hospitali nimewekewa ma dripu tazama pembeni jamaa yangu yule wa migodi nimekaa hospitali siku sita

Nilivyokuwa fresh jamaa akaniambia sasa nazani umepata funzo kwenye maisha yako akaacha hom m2 kwaajili ya matumizi akanichukua tukaenda migodi akanipa eneo na kuniambia pambana

Nikatafuta nyoka yaani wafanyakazi lugha za migodi hizo, tukapiga kazi Mungu si asumani nikapata jiwe la pesa ndefu nakumbuka waliungana kama wanunuzi wa madini watatu kuuchukua ule mzigo nikawapa wale nyoka m200 kila mmoja, walikuwa nne nikaenda kwa jamaa akanipa somo jinsi ya kukaa na hela isipukutike hovyo bila kukusudia nakumbuka pesa yote aliniachia ninapo sema pesa ni pesa kweli

Akaniagizia kama Volvo za mizigo 14 hivi za kichina akawa anazisimamia yeye si unajua watu wa nchi hiyi wakijua unapesa ukikoswa na majambazi basi yatakukuta yale ya jamaa wa mtwara na polisi alijinyonga kwa taulo nchi hiyi ni mwiko kuwa na pesa za ghafla basi nikajenga ka nyumba kakisasa kwajili ya wazazi, fungua pub ya nguvu mbinga na dar anzisha kiwanda kidogo cha unga songea hayo yote nimefanya kwa mgongo wa jamaa sikutaka nijulikane kama nina pesa alafu nikamwambia nipe kazi kwenye hiyo kampuni yako nikawa kama dereva mtiifu baada ya wiki tunakutana kwa siri kujadili hali ya uchumi wetu na mpaka sasa hakuna anayejua mm nina shera kwenye kampuni ya jamaa zaidi ya family yangu maisha yangu ya kawaida sana na hata kwenda kwa miguu kazini kawaida kukaa kijiweni kucheza bao draft kawaida yote haya nimejifunza niliyopitia jamaa wanajua mm ni mwajiriwa wa rafiki yake na kuongea ooh alipata hela kachezea mpaka akanywa sumu ila hawajui kinachoendelea sina cha kupoteza ila nimejifunza sio hayo tu kuna mengi ndani yake ambayo ukifuatilia nyuz zangu utawapata japo nilididimia hapa katikati ila nimekaa sawa

Nb kufilisika sio mwisho changa upya karata zako yote yanawezekana mwanaume pambana kisawasawa acha kulia lia sijui ndio basi kazaaaa kubali kufa ukipambana acha kuwaza waza pambana mpaka uache alama kwenye dunia ameen

Na huu ndio ukumbusho wa picha kati ya pesa ambazo tulikuwa tukigawana hukoo machimbo enzi hizoo nikiwa kwa digar na jamaa zangu[emoji116][emoji116]2020View attachment 2098320
 
Japo kuwa humu zingine zina chumvi ila nimejifunza

2019 nikiwa sina lile wala hili kuna jamaa yangu akaniambia twende tukazamie migodi wapi hiyo Msumbiji basi tumefika kule tukapata kisehem tukapiga kama Zari hivi tukapata mzigo kwenda kupiga bei
Umetema kama m630 ukija kupiga pasu mtu mbili kama m300

Tokea hapo tukakataana urafiki kila mtu aliingia njia zake mana jamaa yangu akadai tukawekeze mim nikaona kuzeeshana mapema huku mi nikaenda zangu dar bila kupitia hom

Fika dar mkwanja si upo kwa bank nikakodi gest nzima nikatafuta mabamnsa kwaajili ya ulinzi tafuta pisi kali kama 10 hivi wakiwemo na mastaa wakike watatu nilikaanao pale gest kwa siku 10 na kubakiwa na laki mbili ya nauli ya kurudi hom mbeya fika hom nikala msoto wa ajabu haijawahi tokea toka nije duniani toka anga za mbali mwaka ukapita nakutana na jamaa yangu ana kampuni yake songea ya usafirishaji mizigo scania kama 23 kumbe mwenzangu aliwekeza kule kele kwenye migodi

Sio siri maumivu yalizidi kusikia hivyo nikamwomba anipe nafasi ya udereva kwenye kampuni yake mana nilikuwa nimepitia huko kabla
Kwakuwa tulikuwa kama ndugu

Akaniambia hapana siwezi kukupa nafasi tena asee kusikia hvy maumivu yalizidi nikajiona sifai nimetengwa na dunia baada ya hisia kunishinda nikatafuta sumu ya panya nikaenda mbali kdg na hom nikanywa
Imepita dakika mbili mwili ukaanza kunyong'onyea macho yanaanza poteza nuru machozi yakinilenga nikikumbuka yote niliyoyafanya ,
Nikasema Mungu naomba unisamehe kwa yote niliyokufanyia ambayo hayakukupendeza

Punde si punde nikiwa kwenye hali hiyo akatokea jamaa yupo na kipkpk akawa anasikia kama kilio hivi cha kugurumia sikujua kilichoendelea ila nilijikuta hospitali nimewekewa ma dripu tazama pembeni jamaa yangu yule wa migodi nimekaa hospitali siku sita

Nilivyokuwa fresh jamaa akaniambia sasa nazani umepata funzo kwenye maisha yako akaacha hom m2 kwaajili ya matumizi akanichukua tukaenda migodi akanipa eneo na kuniambia pambana

Nikatafuta nyoka yaani wafanyakazi lugha za migodi hizo, tukapiga kazi Mungu si asumani nikapata jiwe la pesa ndefu nakumbuka waliungana kama wanunuzi wa madini watatu nikawapa jamaa m200 kila mmoja walikuwa nne nikaenda kwa jamaa akanipa somo jinsi ya kukaa na hela isipukutike hovyo bila kukusudia nakumbuka pesa yote aliniachia

Akaniagizia kama Volvo za mizigo 14 hivi za kichina akawa anazisimamia kilichofuatia baada ya miaka mitatu ni siri yangu ila nimejifunza kwa niliyopitia

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Braza c chai kweli
 
Braza c chai kweli
Hapo sasa inategemea na unavyoamini ww msomaji akili itavyokwambia ni hvy hvy ila ukweli wa mambo ninaujua mm mwenyewe nikiwa hapa mgahawa mchana huu nikipata ugali maharagwe na kisamvu bila kusahau kitimoto robo kilo japo cha leo mifupa kikubwa tutafute pesa na pesa haijawahi tosha ukiona umetosheka pesa jua ndio dalili za kuanza kufilisika aya mengine niachie mwenyewe View attachment 2098309
 
Back
Top Bottom