Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Huu uzi kweli kiboko! nilijua ni Mimi mwenyewe kumbe tupo wengi sana.
Nimemaliza chuo kikuu mwaka Jana Basi mzee akanipa M3, M1 nimsaidie kukarabati nyumba yake na zingine nione nafanyia nini, Sasa mimi kweli nyumba yake nikakarabati sasa hela iliyobaki nikawaza nijengee kijumba kwenye kiploti alichonipa nifanye masuala ya ujasiliamali hapo.

Mpaka sahizi lipo pagale lililoezekwa tu, na hela imekata sina ramani niponipo tu, lakini kila nikiangaliaga matofali yalivyopangika kwenye kijumba napata nguvu kwamba angalau sijaipoteza bure Kuna kitu nimefanya.
 

Bora mara mia wewe wengi wetu hela ilikuwepo na sasa haionekani tofauti na wewe hiyo hela inaonekana ilifanya nini na hujapoteza

Wengi wetu hela ilipotelea kwenye hasara na wengine anasa za pombe na ufuska
 
Bora mara mia wewe wengi wetu hela ilikuwepo na sasa haionekani tofauti na wewe hiyo hela inaonekana ilifanya nini na hujapoteza

Wengi wetu hela ilipotelea kwenye hasara na wengine anasa za pombe na ufuska
😂😂😂

Me ponapona yangu ni kwamba pombe sinywi, Kama ningekuwa nakunywa nadhani ningekuwa nimemalizia huko.
 
Tarehe kama ya leo mwaka uliopita nilikuwa na milioni 40 bank
Leo hii cjui hata siku itaishaje Yaan sina uhakika wa Milo mitatu
Pesa hizi
Ilikuaje Mkuu? Ulikula bata au ulifanya biashara ikafeli?
 
ndio maana mimi nakomaa na tudemu twa 30 na msosi 20. huwezi kukuta nafilisika
 
Ha ha ha yan milion tu ikakutia uchizi [emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya biashara zote ila usiingie kwenye riba either kwa kukopa au kukopesha...mwanzo utaona unafanikiwa ila baadae Mungu atakuchapa kofi ambalo hutakuja kulisahau maishani mwako mwote mpak unazama kaburini.RIBA ni LAANA...ukitaka kuangamia fatana na RIBA. BIASHARA imebarikiwa ila RIBA IMELAANIWA.

Hilo ndio kosa lako ulilolifanya mkuu.
 
Wengi wetu tunadhani kuwa tajiri ana haki ya kuibiwa au kudhulumiwa....laa hasha , DHULUMA haijawahi kumuacha mtu salama..iwe umemdhulumu tajiri au maskini..You will pay the price in this world and the hereafter.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…