Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Mkuu pesa za riba uwe unatoa au kupokea hazijawah mwacha mtu salama hata upate kiasi gani zitakuja kukudhalilisha tu at the end
boss hiyo ni fikra zako, kwa taarifa kila biashara unayoiona ni riba....nunua 100 uza 150....hiyo 50 ni riba....mtu anakuja mwenyewe kukopa fedha yako akaifanyie kazi na unataja vigezo vyako bila hila yoyote na anakubali unampa fedha na anarudisha sawa na mlivyokubaliana....hapo dhambi/kosa lipo wapi....(kwa imani hii benki zote zingefilisika)
 
Nilipewaga dola 100 zamani sana na danga limoja hivi aiseee kwa kipindi kile ilikua ela nzuri nikaja nikaila bila kuelewa imepita wap
Nikaja kupewa tena mil1 na hilo hilo danga zamani kidogo nayo haikufanya la maana
Nikaja nikapata danga lingine likanipa m2 nazo nimefanyia kazi haikuzaaa
Tangu wakati huo miaka imepita sitaki tena ela za madanga,nimeolewa na nina tafuta hela kialali
Msiwashangae kina wema hela za kudanga hata upewe bil 1 huwa zinayeyuka
Safi Sana Kama umehacha kudanga.
 
Tuliuza nyumba ya marehenu babu pale kariakoo karibu na faya wajukuu mgao 50ml nakumbuka terminal one lile jengo jekundu na mabenchi tuu.

Nshawai kwenda zenji me na rubani tuu ile company ya costar kama skosei 2000 hiyo

Viduka vya pamba town vilikua vinanijua maaana nikiwa dukani jua wauzaji hata aje AY hawamsikilizi

Nshaenda graduu pale zanaki nikasababisha graduu iharibike coz vurugu kubwa ilitokea mana watoto wote wazuri walikuja nilipokaaa kila mtu anataka nimjue masela wa Azaboy sindio wakamaind kilinuka balaaaaa

Ndio tupo kwenye vikao vya mwisho hapa kumalizia na hii tunakaa maana tumepauka safari hii akili kumkichwa!



Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaahhahaah daah nimecheka sanaa.
 
Pesa mwana haramu, kaburi limefukuliwa tena🤣🤣
 
Atm inajua kudhalisha kama huna heshima na fedha
IMG-20181124-WA0015.jpeg
 
Pole mzeyaaa... Vipi babe bado yupo nawe au ndio kashatafuta kidume mwenye pesa zaidi yako?
 
Back
Top Bottom