Huu uzi ni very interesting.!
Maisha yana milima na mabonde.! Miaka ya 2014- 18 nilikua na pesa nzuri kula sana bata na totoz hapo dsm na company yakutosha. Enzi hizo ni mwendo wa Hennessy, Green label, MOET, JD etc.
Maisha yamenipiga kofi nimerudi zangu mkoani kujipanga upya, nakumbuka pesa nilizochezea kipindi hicho kama ningekua na akiri ya biashara ningekua mbali sana.! Saivi ni mwendo wa kvant, konyagi au prisner ya buku.
Ila nimejifunza mengi na kujua wapi nilikosea (ujana na ulimbukeni ulichangia), kuna investments nafanya najua zikianza kulipa ntakua njema sana kuzidi hata awali Mungu asaidie.!
Mwanaume kwenye maisha ni kupambana tu hamna kukata tamaa, anguka, inuka futa vumbi songa mbele.