Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Daa! Pole sana. Unaweza kudhani una majanga, kumbe kuna wengine wanakumbana na majanga kukuzidi!Aisee hii mikopo iko nzuri na mibaya, nilishawai kuchukuwa M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
Why?Viscous circle. Ukishaingia hapo kutoka ni mtihani.
PoleAisee hii mikopo iko nzuri na mibaya, nilishawai kuchukuwa M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
Shida ilianzia kwenye ID yako, wenye majina kama ID yako mnapenda sana mikopoIlikuwa mwaka 2011 mwezi wa 7 mara yangu ya kwanza kuchukua mkopo benki, Tsh 3m. Ule mkopo niliufanyia biashara vizuri na nikarejesha bila changamoto kubwa ndani ya miezi 6. Wale maafisa mikopo wakafurahia na kunishauri nichukue mwingine wa Tsh 5m. Nikafikiria na baada ya mwezi nikachukua mkopo mwingine. Ikawa kama bahati wakati nachukua mkopo nikawa nimepata tenda ya kushona uniform za shule flani. Nikaona hili ni dili zuri na kwa bahati wateja wangu wakanilipa pesa za advance zaidi ya 90%. Kilichofuata nikaamua nitafute mafundi wazuri Nairobi wanishonee uniform zote. HAPA NDO BALAA LILIPOANZA. Niliingia choo cha kike. Mkenya niliyempa kazi kumbe ni mshenzi mno... kadhulumu watu wengi sana. Ni kweli ofisi anayo na mafundi anao ila kwa bahati mbaya huwa hatimizi makubaliano. Ujinga mwingine niliofanya ni kumlipa karibu hela zake zote.
Hadi shule zinafunguliwa Januari sikuwa nimepeleka nguo yoyote kwa mteja. Basi presha ikaanza kutoka kwa mteja wangu ambaye pia alikuwa anawashiwa moto na wanafunzi + wazazi. Baada ya kusumbuana na mzabuni wangu nikaona isiwe ishu nichukue hela za kwenye biashara yangu niliyoombea mkopo wa 5m ili kupambana na tatizo ambalo lilikuwa limefikia pabaya. Kwa maana nitafute fundi mwingine nitengenezee kwake huku nikiendelea kupambana na huyu wa mwanzo. Changamoto iliyojitokeza tena ikawa kwa muda ule wauza uniform wengine wana kazi zingine nyingi na bei zao zimeshaenda juu. Gharama za nauli nenda rudi Ars - Nrb nazo zikawa zinanipiga kama ngoma.
Hadi kuja kufanikiwa kupeleka nguo angalau kwa 70% tayari kiuchumi nilishayumba hivyo marejesho yakawa yanasuasua. Ninachokumbuka ule mkopo niliotakiwa niwe nimemaliza kulipa kabla hata ya August nilimaliza December kwa mafaini kibao huku nikiwa nimefilisika. Wale maafisa mikopo walijua kuniwashia moto.
Pamoja na yote hayo nilijipanga upya na baada ya miaka kama mitatu nilirudi tena benki na kuchukua mkopo. Ninamshukuru Mungu kwamba ninakopesheka na ninaendelea kuchukua mkopo. Somo kubwa ni kwamba usichukue mkopo kuanzisha biashara.
Ndio hivyo sijui ni mazoea au kujiendekeza. Ukichukua salary advance chances ni kuwa utaendelea kuchukua kila mwaka.Why?
Maisha ya watz kwa kiasi kikubwa yanafananaNdio ujue kwamba maisha ya mtanzania mmoja yanareflect malaki ya watanzania wengine. Kile unachopitia wewe kuna wengine elfu 10 wanapitia the same kwa wakati huo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee, acha kabisaaUkishakauka unakufwazzzz 😄
Pole sana dada yangu , naamini utatokea muujiza wewe mwenyewe hutaamini .Nina mkopo wa 1M point...
Leo natakiwa nianze rejesho ila pesa yote imeishia kwenye harus
Nawazaaaaa
Miujuza itendeke tuu
Nafkri na Mimi nifanye hivyo. For real nateseka sana. Yaani kesho niende kuongea nao mkopo usimame wenyewe bila riba. Waki goma hata mahakamn wanifunge tu[emoji24].Pole sana. Hii ilishawahi kunikuta ila nilichofanya ni kulipa nusu nusu kama miezi miwili deni likaisha. Hapo nilishalipa riba kama miezi 4
Kama unazungusha Haina shida, unalipanataka kuchukua mkopo wa 20m ninunue gari ...nitaweka hati ya nyumba kama dhamana....hii blanda ndio plan yangu
Kwa sababu 100% n real life kwa groundUzuri wa Jf kila ukiletwa uzi humu hakuna asiyejua ,,kila mtu kapitia au anapitia hakuna aliye mzembe ,wala asiyejua kila kitu,,,,.
Acha kabisa mkuu,Mwanangu DeepPond hata mimi kuanzia September sielewi kabisa. Rejesho langu 3m napata kichaa
Sio Siri. Mkop utakua mzuri if mambo yakienda vzr. Ila ikiwa vice versa utajuta. Kuna muda mtu anakusemesha badala ya kumjibu una jichekesha kwa stressAcha kabisa mkuu,
Mimi nishapunguzahata Kasi ya kuagiza mzigo,
Usipoenda kwa timing
Unajikuta una mzigo mkubwa dukan na wateja hamna na hapo hapo unadaiwa rejesho.
Mwisho wa siku unajikuta unajumlisha mzigo kwa Bei ya hasara ili upate rejesho
Pole saa mkuu,Mimi nilikopa laki 5 kwa riba ya 20%. Ilikua mwaka Jana huez amini mpaka Leo sija maliza napeleka riba tu. Nasogeza rejesho mbele[emoji24][emoji24] sjui nitatokaje hapa na mishe ndo kama Zina nigomea hivi
Dah! Pole sanaNiliwahi mdhamini mtu black akakimbia ..marejesho yakawa juu yangu na wakati huo Nina setback ya maana[emoji23][emoji23]nilitamani ardhi ipasuke.. nashukuru nilimaliza ila Cha Moto nilikiona
Wanaudhi balaa,Mimi tangia August sielewi naona nyota nyota tu!,ila mwenyezi Mungu ni mwema atanifanyia wepesi inshaallah!,ila watu wa benk wanapiga simu hadi natamani nitie block wote [emoji851]
Sahii kabisa umemuelimisha,Ndio ujue kwamba maisha ya mtanzania mmoja yanareflect malaki ya watanzania wengine. Kile unachopitia wewe kuna wengine elfu 10 wanapitia the same kwa wakati huo.
Sent using Jamii Forums mobile app