Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Mimi nilikopa milioni 8 ada na meals. Nikanunua kiwanja 3m. Nyingine matumizi kidogo na ada. Kile kiwanja nilichonunua miaka 12 nyuma leo thamani yake ni 50m.
HESLB nawalipa kila mwezi hela yao 30,000.

Asante sirikali.
Mkuu walikuwekea 8m cash kwenye account yako?
 
nakopa zngu kwa ndugu jamaa na marafiki..
Hamna marejesho , tutalipana mbele kwa mbele
 
Mithali 22:7
"Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye".

Nikasema nisome biblia inifariji ndo nikakutana na huo mstari. πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ™ŒπŸ™Œ
Nimecheka
 
Una marafiki wazuri.
 
Hahaaa.. Wanasema gari yako dhamana yako.. watu wanatembezwa kwa miguu sana
Ilifana [emoji23][emoji23][emoji23]
Vile umechukua zako jiko la mkaa..ghafla yanakuja majiko ya gesi..
 
🀣🀣🀣🀣
 
mazaa alikua akichukua mikopo kwa wale SEDA.. asee mambo yakaenda kombo akawa anawatoroka maana anajua siku zao za doria..

Wakaja kwa kushtukiza kwetu ni badland kule gari unaacha road upite chocho kadhaa ndo ufike..

Braza alikua anajua ile gari ya alivyoiona chap mbiombio akaja kumshtua maza, chap akazama uvunguni..

Wakafika cha kwanza..mama yuko wapi ? Braza kwaambia amesafiri kuna msiba kijjini alikua anajibu kwa wasiwasi..

Mmoja wao akanichukua nlikua ndo niko Darasa la kwanza haoo hadi dukani...Mangi mpe mtoto mzuri biskuti ilikia zile za choclate 500/=nakumbuka..

Woii nikachoma maza yupo uvunguni kule.. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ wakaenda kumchomoa, hela hamna wakasomba mazaga hapo sebleni

Ile kipigo nlipata walivyoondoka biskuti ilitokea puani...
 
hii mikopo kausha damu balaa sana mam yangu alichukua pesa kidogotu kama laki tatu hivi kila siku analipa 5 elfu amekauka apa na mkopo hauishi anafanya kulipa faini tu mkopo upo pale pale Ni huzuni kwa kweli nimeuza mpaka kitanda kumsaidia
Me nahisi huu mkopo bi mkubwa wangu atakuwa kakopa si bure mana anaomba ela balaa sio kawaida yaan mfn mwezi uliopita kaniomba ela ya bill ya dawasco mara 3
Nikampa tu ila nikahisi kitu
Hii mikopo inawaathili sana wakinamama
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me nahisi huu mkopo bi mkubwa wangu atakuwa kakopa si bure mana anaomba ela balaa sio kawaida yaan mfn mwezi uliopita kaniomba ela ya bill ya dawasco mara 3
Nikampa tu ila nikahisi kitu
Hii mikopo inawaathili sana wakinamama
Ubaya wanakopa kwa kausha damu si chini ya wawili mtiti ndio huazia hapo.

Ila kausha damu mmoja fresh unaweza kummudu
 
Kuanzia mwaka huu nimeamua kuchukua mkopo wa biashara badala ya kazini. Hapa nina kipengele cha 10m Nmb nimeshafanya marejesho mawili.

Kilichonivutia ni riba yaani nimeona kwenye mkopo wa biashara 10m nalipa 11,300,000/= kwa mwaka. Kwa mwezi 946,000/=. Wakati mkopo wa kazi muda mrefu na riba inakuwa kubwa.

Ninachofanya kazini nimeweka backup kama nitafeli huku basi nitazama kwa mkopo wa kazi kurefund. Lakini piashara ninayofanya ni ya fedha kwa hiyo fedha zote ninazo cash ninachowarudishia ni faida tu. Kinachonipa matumaini ni kuwa kwa vile cash zao zote zipo kama nitaona nafeli nazirudisha, sokomoko itakuwa kama zitaibwa au changamoto zingine unexpected.

Nashukuru Mungu 10m zao zinanipa at least 2.3m monthly profit nawapa rejesho na kuongeza mtaji. Kwa hiyo bado sina neno baya juu ya mkopo cha msingi nipo highly disciplined and very cautious, hata wife ananikubali katika heshima juu ya that why hajasita kuweka saini za mkopo na kuacha hati ya banda letu. Niombeeni nitoboe mwakani nivute 20m[emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ha ha yan faida unajipangia mwenyewe [emoji3][emoji3]
Hata sisi kabla hatujachukua mkopo tulikuwa na mawazo kama yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…