Hawa watu hasa wa microfinance wanakwaza sana
Na siku ya mwishobwatakua wanachomwa kama hotdog wanaviringishwa ndani ya gogo af wanaunguzwa taratibu waahed kabisa.
Kuna mmoja alikuja kazini amechomekea mpka kwenye diaphram na hesima deebe ananidedesa nichukue mkopo kwao marejesho yao ni kidogo hayaumizi. Nkamwambia aende aniachie kipeperushi nitafakari. Alivoondoka nkakaa nkapiga hesabu vzuri kbsa taratibu, nkaja kushtukia kua naenda kupigwa riba ya almost 30% kisirisiri, nkachana kipeperushi nkatupa kwenye dustbin.
Jamaa hakuogopa akaenda kwa mlinzi wa ofisi akamseti, msukuma wa watu akajaa kingi akachukua mkopo kwa kuamini kua rejesho la elf 5 kwa wiki hawezi kosa. Baadae akaja nkampigia hesabu nkamfungulia dunia kama clouds fm, alichoka. Yuke mlinzi kila jembe analopiga ardhini anawatukana wale jamaa. Alifanikiwa kulipa lkn kwa uchungu sana.
Bora nikope kwenye vikundi vya hisa huko, yakinishinda wanachukua hisa zangu aibu inapungua.