Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Aka siwajui mimi
Naskia kuba asa, kausha damu na chupi mkononi
Umefiwa na nani na uko wapi?
Nimefiwa na Dada yangu Mkuu nipo DSM,natafuta mkopo wa laki 3 nina laptop yenye thamani ya 1.8 kama dhamana but hela nitairudisha kabla ya tarehe 25 ya mwezi huu.
 
Nimefiwa na Dada yangu Mkuu nipo DSM,natafuta mkopo wa laki 3 nina laptop yenye thamani ya 1.8 kama dhamana but hela nitairudisha kabla ya tarehe 25 ya mwezi huu.
Pole sana kwa msiba mkuu, hope utapata mkopo huo. Hata nyuma ya keyboard tujitahidi kuishi na watu vizuri sababu hujui utamuhitaji nani, kwa wakati gani. My condolences to you and ur family.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefiwa na Dada yangu Mkuu nipo DSM,natafuta mkopo wa laki 3 nina laptop yenye thamani ya 1.8 kama dhamana but hela nitairudisha kabla ya tarehe 25 ya mwezi huu.
Nichek inbox tuyajenge tusaidiane
 
Aisee hii mikopo iko mizuri na mibaya, nilishawahi kuchukua M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
Pole sana.
 
Dadangu anafosi nimwandikie barua ya mkopo,
Anakopea kiwanja cha urithi, hii ni mali yetu mimi na yeye....hii pesa nina wasiwasi hatarudisha.
Naandika kesho kuepuka lawama ila najua ili deni nitalipa mimi dadeki.
Kama bado hujaandika usiandike hiyo barua. Mwambie atafute nusu utamwongezea. Akishapata nusu biashara imeisha.
 
Miradi ya serikali noma sana. Watu ambao walifanya kazi enzi za JK halafu malipo yao yakakutana na uongozi wa JPM walilizwa mno. Kuna jamaa yangu Kigoma alikuwa kashapiga hatua aliishia kufilisika mazima. Ukiwa unafanya project.ya serikali inahitaji umakini.
Yule wa ujenzi?
 
Mkopo wa MGODI voda, nilikopa siku nataka kulipa mtandao ukasumbua. Nikasema itakula kwenu leo kesho yake wakaanza meseji zao Mimi nimetulia tu.

Zikapita siku kadhaa, si Kuna bwege kanipigia kwa namba 100 ananikoromea kisa 3,600. Nilichomjibu akanifungia huduma ya mpesa. Kesho yake naweka elfu 2 bila kujua kumbe kaifunga, nawapigia simu wananiambia nilipigiwa simu nikawajibu vibaya kwa hiyo niende voda shop na kitambulisho.

Nikawaambia laini ninazo nyingi sina huo muda wa mchezo, nikaitoa nikaivunja nikaweka ya tigo.
Hahaaa
 
Hawa watu hasa wa microfinance wanakwaza sana
Na siku ya mwishobwatakua wanachomwa kama hotdog wanaviringishwa ndani ya gogo af wanaunguzwa taratibu waahed kabisa.

Kuna mmoja alikuja kazini amechomekea mpka kwenye diaphram na hesima deebe ananidedesa nichukue mkopo kwao marejesho yao ni kidogo hayaumizi. Nkamwambia aende aniachie kipeperushi nitafakari. Alivoondoka nkakaa nkapiga hesabu vzuri kbsa taratibu, nkaja kushtukia kua naenda kupigwa riba ya almost 30% kisirisiri, nkachana kipeperushi nkatupa kwenye dustbin.

Jamaa hakuogopa akaenda kwa mlinzi wa ofisi akamseti, msukuma wa watu akajaa kingi akachukua mkopo kwa kuamini kua rejesho la elf 5 kwa wiki hawezi kosa. Baadae akaja nkampigia hesabu nkamfungulia dunia kama clouds fm, alichoka. Yuke mlinzi kila jembe analopiga ardhini anawatukana wale jamaa. Alifanikiwa kulipa lkn kwa uchungu sana.

Bora nikope kwenye vikundi vya hisa huko, yakinishinda wanachukua hisa zangu aibu inapungua.
Unajua uandishi wako umenichekesha hahaaaaaaa
 
hii mikopo kausha damu balaa sana mam yangu alichukua pesa kidogotu kama laki tatu hivi kila siku analipa 5 elfu amekauka apa na mkopo hauishi anafanya kulipa faini tu mkopo upo pale pale Ni huzuni kwa kweli nimeuza mpaka kitanda kumsaidia
Sasa unalala wapi? Au ulikuwa na vitanda viwili?
Hahaaaaaa
 
Nimefiwa na Dada yangu Mkuu nipo DSM,natafuta mkopo wa laki 3 nina laptop yenye thamani ya 1.8 kama dhamana but hela nitairudisha kabla ya tarehe 25 ya mwezi huu.
Laptop aina gani?..weka bond uje nikupe laki 2
 
Mzee wenu anawadanganya,kwanza wanafacitate malipo ni NSSF/PSSSF hazina Nazi yao ni kutoa hela tu.hata kama mstaafu hajahakikiwa hela wanamuingizia kama kawaida.
Hapana lazima kila baada ya miaka mitatu aende aka akikiwe kama bado yupo hai, Serikal siyo wajinga ilipe tu pesa bila kujua mstaafu yupo au ameshafariki, ndiyo maana kila baada ya kipindi fulani wanatakiwa waende Azina waka akikiwe kama bado wapo hai, na kama hasipo enda Azina hawezi kumuingiza pesa wana jua amefarki
 
Back
Top Bottom