Tuliowahi kuwa na chawa tukutane hapa

muuza ubuyu

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
3,539
Reaction score
3,551
Mambo vipi watemi?

Ebanaee tulio wahi kuwa na chawa tukutane hapa tubadilishane uzoefu. Binafsi nilipokuwa mdogo mpaka darasa la pili nilikuwa na chawa wengi sana kiasi kwamba kichwa kilikuwa cheupe kama mvi kwa sababu ya mayai ya chawa. Basi bibi alikuwa ananiita halafu anazitafuna nywele zangu ili kuvunja mayai ya chawa.

Vipi uzoefu wako!
 
Duuuhhhh ngoja nitanie kidogo!!!!!

Mara nyingi ,,chawa ,,kunguni ,,mende ,panya ,,,huwa vinaelezea familia malezi ya MTU alokulia.
Hahahahaaaaa, hilo silo la kuuliza. Hata mtu akikngelea BMW, Benz, harrier, Nissan, jakuzi, swimming pool n.k navyo vinaelezea mazingira aliyokulia mtu.
Na nimeamini kulingana na heading ya uzi huu na wewe ulishawahi kuwa na chawa!
 
HAHAHAHA umenikumbusha kisa cha jana kwenye daladala tulikumbana na kunguni
 
Chawa wakoje??
 
Mi nilikuwa naishi kigeto geto na wajomba zangu toka nikiwa mdogo. Nakumbuka miaka ile ya 2000s wajomba walikuwa wanapendeza sana kimavazi wakati tulikuwa tunalala kwenye godoro lenye size ya ulimi wa mbwa na limejaa kunguni na mayai yao kila baada ya sentimita mbili unakutana na koloni la kunguni.

Siku moja nmekaa na wajomba zangu kunguni akapita kwenye zipu ya mmoja wa anko zangu.. Wote tuliopale tukamuona kasoro yeye tu, tulipo mshtua jamaa kwamba anakunguni anazinguka zunguka eneo la nyeti, jamaa alitushangaza kwa kusema "muacheni kunguni wangu mwenyewe namfuga akue akue ! " tulicheka sana kwakweli...!
 
Hizi trends za threads za TUKUTANE HAPA zinaelekea kubaya sasa...mwishowee hadi mashoga nao watasema tukutane hapa
Mkuu, ya mashoga labda uianzishe wewe! Halafu nadhani hujui hili ni jukwaa gani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…