G
guest-1787677255
Guest
Mhhhhh kuna harufu ya chai hapa.Wakuu, kwanza sitaki kusema kwamba kutumia Dawa ni jambo baya ni jambo zuri sana ila unapotumia Dawa hakikisha unatumia km ulivyoelekezwa na Mtoa Huduma ya Afya.
Kisa changu ni hiki:
Siku hio ilikua Mwaka huu Mwanzoni km January hivi kwenda February, nilijihisi sipo sawa kifua kinabana na hali ya kupumua haipo sawa. Sasa mimi kuna Dawa hua nachukua pharmacy fulani hizo Dawa ni za kifua na mafua hua nazitumia mara nyingi nikiwa sipo sawa na nimekua ninazitumia na zinanisaidia na natakiwa kutumia KIDONGE kimoja tu kwa saa 24.
Siku hio bwana hali ilikua mbaya sana kifua kimebana nashindwa kupumua na zile Dawa nilikua nikinywa kimoja tu kifua kinafunguka naanza kuhisi napumua vizuri kabisa.
Siku hio nimenunua km VIDONGE 4 pale nimeelekezwa ni KIDONGE kimoja ×1. Nikanywa kimoja sasa VIDONGE vyenyewe ni km PIPI tu vitamu ila unaweka mdomoni humezi unamung'unya km Chocolate mpaka kiishe ukivuta hewa unaanza kuona kifua kinaachia na unaanza kupumua vizuri.
Sasa hio siku nilikua najisikia vibaya sana nimekula KIDONGE cha kwanza hali bado ikawa tete nikasema leo hapana hata km ni 1×1 ngoja nitumbukize KIDONGE cha pili nikapiga cha pili, nimekaa nikihisi labda hali itakaa sawa wapi nikaongeza KIDONGE cha tatu, kumbuka ni 1×1. Kikabakia KIDONGE Kimoja kati ya VIDONGE Vinne.
BAADA YA HAPO SIKUAMKA BAADA YA MASAA 24. NILILALA KITANDANI WIKI NZIMA KUANZIA JUMATATU MPAKA NIMEKUJA KUPATA UHUHENI NA NAFUU NI JUMAMOSA KWENDA JUMAPILI NI MIMI NA KITANDA TU MWILI ULICHOKA WOOTE, KUTEMBEA NILIKUA SIWEZI, KIZUNGUZUNGU SIO KIZUNGUZUNGU SIELEWI.
USIJI-OVER DOSE NI MBAYA SANA WAKUU.
Je! Wewe ulipoji-overdose ulijisikiaje? Tuelezee na sisi mkuu.