G
Mhhhhh kuna harufu ya chai hapa.Wakuu, kwanza sitaki kusema kwamba kutumia Dawa ni jambo baya ni jambo zuri sana ila unapotumia Dawa hakikisha unatumia km ulivyoelekezwa na Mtoa Huduma ya Afya.
Kisa changu ni hiki:
Siku hio ilikua Mwaka huu Mwanzoni km January hivi kwenda February, nilijihisi sipo sawa kifua kinabana na hali ya kupumua haipo sawa. Sasa mimi kuna Dawa hua nachukua pharmacy fulani hizo Dawa ni za kifua na mafua hua nazitumia mara nyingi nikiwa sipo sawa na nimekua ninazitumia na zinanisaidia na natakiwa kutumia KIDONGE kimoja tu kwa saa 24.
Siku hio bwana hali ilikua mbaya sana kifua kimebana nashindwa kupumua na zile Dawa nilikua nikinywa kimoja tu kifua kinafunguka naanza kuhisi napumua vizuri kabisa.
Siku hio nimenunua km VIDONGE 4 pale nimeelekezwa ni KIDONGE kimoja ×1. Nikanywa kimoja sasa VIDONGE vyenyewe ni km PIPI tu vitamu ila unaweka mdomoni humezi unamung'unya km Chocolate mpaka kiishe ukivuta hewa unaanza kuona kifua kinaachia na unaanza kupumua vizuri.
Sasa hio siku nilikua najisikia vibaya sana nimekula KIDONGE cha kwanza hali bado ikawa tete nikasema leo hapana hata km ni 1×1 ngoja nitumbukize KIDONGE cha pili nikapiga cha pili, nimekaa nikihisi labda hali itakaa sawa wapi nikaongeza KIDONGE cha tatu, kumbuka ni 1×1. Kikabakia KIDONGE Kimoja kati ya VIDONGE Vinne.
BAADA YA HAPO SIKUAMKA BAADA YA MASAA 24. NILILALA KITANDANI WIKI NZIMA KUANZIA JUMATATU MPAKA NIMEKUJA KUPATA UHUHENI NA NAFUU NI JUMAMOSA KWENDA JUMAPILI NI MIMI NA KITANDA TU MWILI ULICHOKA WOOTE, KUTEMBEA NILIKUA SIWEZI, KIZUNGUZUNGU SIO KIZUNGUZUNGU SIELEWI.
USIJI-OVER DOSE NI MBAYA SANA WAKUU.
Je! Wewe ulipoji-overdose ulijisikiaje? Tuelezee na sisi mkuu.
Sawa mjumbe uzingatie siku nyingineMimi ni mzee wa miti shamba Kuna day nilihisi mwili haupo sawa Sasa nikanywa mwarobaini ila baadae nikasahau nikameza pirton 2 hapo ndo niliona Dunia ikizunguka Kwa macho yangu
Hapo bila kujua jina la dawa siwezi kuelewa chochote Mkuu...Ni KIDONGE cha mafua au kifua kinauzwa KIDONGE kimoja 500, hio dawa ina nguvu sio kawaida yaan ukinywa hapo hapo inaanza kufanya kazi hapo hapo ninapokwambia kifua kikibana na nikihisi km nashindwa kupumua nikichukua kimoja tu nikaanza kumung'unya kifua kinaacha kubana na naanza kupumua vizuri tu, maduka mengi ya pharmacy huwezi kukikuta ni duka hilo tu ndio analetaga, kuna siku moja nilienda nikakuta vimeisha zunguka pharmacy zote hawana na hawaijui kabisa
Eeeh hii dawa kumbe ipo ya vidonge,,mi nilikua natumia kwa mwanangu,siku naenda nunua nkakuta dok mwingine kuuliza umri wa mwanangu nkamtajia akagoma kunipa,, kumbe ni balaaAndika Google "ZECUF" utakiona, usije ukathubutu ukala vingi sio pipi hizo mkuu, ni vitamu ila usile vingi sio pipi kula kimoja kaa masaa 24 ndio ule kingine ukila vingi usinitaje
View attachment 3416092
Nasema cha chiniKipi na kipi mkuu?
Nimekuelewa Mkuu...ZECUF nimeweka hapo juu mkuu nilizidisha DOZI usije ukajaribu kuthibitishaView attachment 3416192
nilkua nachukulia kawaida sababu dawa zingine zote zilikua zinadunda,ila io ilikua fungakazi kwaio nikaipenda mnoooKumbe ulikua hujui hii dawa mkuu?
Dah nimecheka sana kama fala vileNlienda kupma nkaambiwa na marelia nkachukua Alu zile dawa mseto za marelia na panado nkanywa 4 usku ile asubh nkanywa saa kumi na mbil v4 tena nkarud kulala kuja kuamka saa mbil nkasahau kama nlkunywa nkavuta vingne 4 nkameza ndan ya nusu saaa nkaanza kuona kama mambo hayako sawa kizungu zungu miguu inakosa nguvu naskia kama magoti yanaliwa na mchwa naona kama ndan giza linaingia nkasema hii dawa itakua kal au marelia imepanda zaid nkamwta dogo em niesabie hizo dawa akaniulza ulianza lin nkamwambia jana usku sasa mbona zshatumika 12 apo ndio kchwa klpata moto akakimbilia maziwa fasta m najitapsha wap yanatoka maji tu nkapewa maziwa na kupelekwa hsptal nkapewa ktanda na drp nkazima mpaka saa tatu usku ndio nakuja kuznduka njaaa hata.. kimsng uspopta msaada wa haraka unakata moto
Uongoooo huooooMimi nilijiaoverdose nikaishia kutapika vidonge vyote nilivyomeza
HayaUongoooo huoooo