Naona thread ina takribani wiki moja... kabla UBS AG hawajatangaza kuichukua Credit Suisse!Mkuu Chige tafadhali njoo useme chochote hapa.
Na hapa tusisahau kwamba, ingawaje CS ni miongoni mwa largest investment banks duniani, UBS kwa upande wake ni DUDE ingawaje "udude" wake haukufanya CS washindwe ku-compete nae globally.
Na hapa ukumbuke, kabla ya 1990's, UBS likuwa ndo benki kubwa zaidi Uswisi. Katikati ya miaka ya 90, kuna benki nyingine kubwa huko huko Uswisi (nimeisahau jina) ikakumbana na hiki ambacho CS kimewakumba hivi sasa.
Ikaibuka ligi kati ya CS na UBS kutaka kuinunua hiyo benki. Dakika ya 90, CS wakawapiga bao UBS, na ufalme wa UBS kwa CS ukaenda likizo na hatimae CS kuwa ndie largest investment bank in Uswisi.
Nadhani katika kujaribu kurejesha taji lake la ufalme wa kibenki, miaka michache baadae UBS wakaanza kununua vibenki vidogo vidogo lakini haikuwasaidia. Mbaya zaidi, UBS nao wakaja kukumbwa na management vs investors crisis.
Like in any other capitalist world, CS wakataka kutumia fursa kuinunua UBS lakini wakatolewa nje.
Nadhani tena katika harakati zile zile za kurejesha ufalme, miaka michache baadae UBS wakaungana na benki nyingine kubwa ya Uswisi (among Top 5).
Muungano huu ukaifanya CS kutupwa tena nje ya Kiti cha Ufalme manake ndio muungano uliozaa Dude lingine kubwa zaidi sio tu ndani ya Uswisi bali Duniani.
Leo hii, yule CS ambae alifanya attempt ya kummeza UBS, hatimae ni yeye ndie miguu yake tayari imeshatangulia mdomoni mwa UBS, na HANA namna ya kuchomoka!!
Tafsiri ya maelezo hayo hapo juu ni kwamba, endapo deal la UBS na CS litakamilika basi Wawekezaji na Wateja wa CS hawana tena sababu ya kuhofia.
Wateja hao hawatakuwa na sababu ya kuhofia kwa sababu hatimae watakuwa chini ya DUDE moja KUBWA MNO! Dude ambalo litakuwa limeshameza moja ya Washindani wake wakubwa internationally and domestically-- means, more businesses!
Lakini kwa upande mwingine, Mshindani MKUBWA wa UBS kwenye Soko la Uswisi ni mabenki yaliyo chini ya serikali ya Uswisi ingawaje CS nao walikuwepo.
Sasa kwa kuwa UBS wataichukua CS, maana yake ni kwamba CS Businesses (I mean Wateja) NDANI ya Uswis zinageuka kuwa UBS Businesses. Kutokana na hilo, UBS atakuwa ameongeza nguvu za kiushindani dhidi ya Mabenki ya Serikali kwenye soko la Uswis.
Hapo juu ni faida nyingine kwa desparate CS Customers kwa sababu, more and more businesses! Bank ikiongeza biashara, ni faida kwa Wateja na Wawekezaji. Of course, kwa Mteja ambae sio Mwekezaji faida ni ile confidence kwamba pesa yake ipo safe.
Anyway, lakini na CS wenyewe walikuwa ni watu wa ovyo sana kwenye utoaji wao wa mikopo hususani kwa Africa. Hawa jamaa walikuwa very corrupt, na ukiona benki inapata lending business through corruption, fahamu hiyo corruption ni sehemu ya Cost of Doing Business, na kwahiyo inakuwa compensated kwa namna nyingine kama vile riba kubwa, and the like.