Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Katika ujana wangu, nilikuwa mlafi sana; nilikuwa nikiona tu pisi kali inayoshawishi na kuuteka moyo wangu, nitaanzisha naye mahusiano na hatimaye tunajikuta tayari tuna mtoto; ingawa tangu mwanzoni huwa nawaambia mimi ni mme wa mtu,lakini wao hawajali.
Hii imenipelekea kuwa na watoto 6 nje, kila mmoja na mama yake; wapo walimbwende walionizidi urefu, wengine wana viuno vya nyugwi (umbo namba 8) n.k;
Kutokana na uzuri wao, nilikuwa natumia gharama kubwa angalau niweke alama ya mtoto, ili huko mbeleni iwe rahisi kupasha kiporo pale ninapohitaji.
Changamoto ninazokutana nazo:-

- Hawa wazazi kutaka tuendelee kula bata kama nilipokuwa kijana, wakati sasa na uzee wangu huu majukumu yameniandama na kuamua kupunguza baadhi ya starehe. Hii imepelekea wengine kuvunja mawasiliano na mimi; ingawa najua huko mbeleni watoto wakikua watanitafuta.
- Wengine wanataka wapindue ndoa ili wao watambulike kama mke, bahati nzuri hilo nimeweza kulidhibiti (hapa nimeweza kuwazidi wavamizi wa M23).
- Wengine kuzidisha bili kwenye mahitaji ya mtoto, lakini hili pia nimeweza kulidhibiti.
Mafanikio:-
- Bi mkubwa hajui kama nina watoto nje; na hii nataka iwe siri mpaka hao watoto wote wawe sekondari nasi tukiwa kwenye umri wa busara ndio tuweze kuzungumza.
- Nategemea huko mbeleni nikiwa mzee sana, nitakuwa nimezungukwa na vijana wangu wasiopungua 11.
- Kupata huduma ya tendo iwapo mmoja wapo ataamua kuzingua.
Karibuni kwa uzoefu