Tuliozaa nje ya ndoa tukutane hapa, tujadili changamoto tunazokutana nazo

Tuliozaa nje ya ndoa tukutane hapa, tujadili changamoto tunazokutana nazo

Jitahidi mali ya bi mkubwa iwe yake na familia yake. Hao wengine wape mali zao au jenga moja kwa ajili yao na uandike.
Tàtizo nu hawa wanaume wanaooa hawa wanawake tuliozaa nao. Kuna mmoja kapiga marufuku mawasiliano na mzazi mwenzangu anadai anahudumia mama na mtoto. Sasa mawasiliano hadi aende kazini. Mliooa single maza mjue tunawasiliana nao hata kama umekataza.
 
Katika ujana wangu, nilikuwa mlafi sana; nilikuwa nikiona tu pisi kali inayoshawishi na kuuteka moyo wangu, nitaanzisha naye mahusiano na hatimaye tunajikuta tayari tuna mtoto; ingawa tangu mwanzoni huwa nawaambia mimi ni mme wa mtu,lakini wao hawajali.

Hii imenipelekea kuwa na watoto 6 nje, kila mmoja na mama yake; wapo walimbwende walionizidi urefu, wengine wana viuno vya nyugwi (umbo namba 8) n.k;

Kutokana na uzuri wao, nilikuwa natumia gharama kubwa angalau niweke alama ya mtoto, ili huko mbeleni iwe rahisi kupasha kiporo pale ninapohitaji.

Changamoto ninazokutana nazo:-​
  • Hawa wazazi kutaka tuendelee kula bata kama nilipokuwa kijana, wakati sasa na uzee wangu huu majukumu yameniandama na kuamua kupunguza baadhi ya starehe. Hii imepelekea wengine kuvunja mawasiliano na mimi; ingawa najua huko mbeleni watoto wakikua watanitafuta.​
  • Wengine wanataka wapindue ndoa ili wao watambulike kama mke, bahati nzuri hilo nimeweza kulidhibiti (hapa nimeweza kuwazidi wavamizi wa M23).​
  • Wengine kuzidisha bili kwenye mahitaji ya mtoto, lakini hili pia nimeweza kulidhibiti.​

Mafanikio:-​
  • Bi mkubwa hajui kama nina watoto nje; na hii nataka iwe siri mpaka hao watoto wote wawe sekondari nasi tukiwa kwenye umri wa busara ndio tuweze kuzungumza.​
  • Nategemea huko mbeleni nikiwa mzee sana, nitakuwa nimezungukwa na vijana wangu wasiopungua 11.​
  • Kupata huduma ya tendo iwapo mmoja wapo ataamua kuzingua.​

Karibuni kwa uzoefu​
Mm ninao wanne , watatu ni halali kabisa ila wanne mama yake mwaka jana kaniambia tukapime DNA maana wakati anabeba mimba alichanganya wanaume namm nikiwemo kwenye ule mchanganyiko kwahiyo nina safar mwezi wa tatu tukapime
 
Hakuna asiyependa kuwa na watoto
Hii dunia kanuni zake mkuu, na ukiishi kwa hizo kanuni hakuna tatizo shida inakuja watu wanaongozwa na hisia zaid. Huwez kumzalisha mtoto wa mtu ahalafu uone ni sawa kisa wanataka wenyewe. Lazima uwe na kiasi. Ukitaka familia imara generation iliyonyooka. Lazima wakati mwingine tujifunze kuacha ubinafsi. Hao watoto kawaida wanalishwa sumu tofauti tofauti kulingna na mama zao. Wakikua watu wazima hawataelewana tena. Na ndio dunia unairabu. Huku wamama umewafanya wazinzi kule kizazi cha chuki. Hayo yote ya nini
 
Back
Top Bottom