new forest
Member
- Mar 28, 2024
- 35
- 97
Pamoja na changamoto mbalimbali tunazo kumbana nazo katika harakati za safari ya maisha, lakini ndiyo Raha ya safari. Maisha yangekuwa yamenyooka tu bila changamoto za hapa na pale, sidhani kama tungefurahia maisha. Changamoto ndio Raha ya safari ya maisha na ndio zinafanya Dunia unakuwa na mengi ya kusimulia na kusimulia.
Nimeleta Uzi huu special Kwa wahenga wenzangu TULIOZALIWA miaka ya tisini. Kama ukiniuliza Mimi nitakwambia nyakati zile pamoja na kwamba ulimwengu WA digatali ulikuwa bado sana Ili TULI- ENJOY sana maisha ya nyakati zile pamoja na changamoto za analogy, Leo nitawakumbusha baadhi ya nyakati,
Nani anakumbuka namna tulivyokuwa tunasubiri Kwa hamu siku ya jumamosi.
Yaani Jumamosi ilikuwa inasubiriwa Kwa hamu kuanzia mchana, tunaangalia marudio ya wiki nzima ya michezo ya kaole, pale ITV. Alafu jumamosi hiyo hiyo usiku baada tu ya taarifa ya habari tunasubiri mchezo WA kaole. ENZI hizo kuna tamthiliya kama, Gharika, Tufani, Taswira, Fukuto, Safari nk.
Yani ilikuwa balaa. Na Yale maigizo yalikuwa yanakutanisha familia pamoja coz hakukuwa na "access" ya internet kama ilivyo sasa, haikuwa rahisi kuyaona Yale maigizo sehemu tofauti na kwenye television tu. Coz hakukuwa na smart phone na matumizi ya computer yalikuwa zaidi kwenye ofisi za serikali.
Nani anakumbuka ENZI zile tunaenda kuangalia sinema kwenye "video shows"?. Wengi wetu hatukuwa na TV nyumbani, hivyo sinema nyingi tulikuwa tunaenda kuangalia video show, Kwa shilingi mia. Nakumbuka ENZI hizo mikanda ndio ilikuwa inatumika, hivyo ilikuwa ukipita nje ya video show unakuta wamebandika makava ya mikanda itakyoonyeshwa siku hiyo na muda. Nakumbuka baadhi ya video show kulikuwa kuna jamaa anawafafanulia hizo tamthiliya hasa zile za kizungu, na nigeria zilizokuwa zinatamba KIPINDI hicho.
Bongo muvi ilikuwa bado bado. Nakumbuka bongo muvi ilikuja kuanza miaka ya 2003, hasa baada ya musa Banzi kutoa filamu ya Nsyuka, amabayo ndio ilikuwa ya kwanza ya kichawi, baada ya hapo ndo wengine wakaanza.
Hivyo nathubutu kusema pamoja na changamoto za ENZI zile za analogy, ila kuna namba TULI- enjoy sana maisha tofauti na zama hizi za digital.