Tuliozaliwa Dar na kukulia Dar, mara ya kwanza kwenda kijijini ilikuaje?

Tuliozaliwa Dar na kukulia Dar, mara ya kwanza kwenda kijijini ilikuaje?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu,

Tumesikia na tunaendelea kusikia story nyingi vituko na mikasa inayosimuliwa na watu wanaokuwa wamefika Dar kwa mara ya kwanza, jinsi jiji lilivyowakaribisha na kupata ile maana halisi ya msemo "Mjini shule".

Sasa tusikie kwa upande wa Dar na experience zao walivyofika kijijini kwa mara ya kwanza ilikuwaje.

Nini yalikuwa matarajio yako? Nini kilikushangaza na somo gani ulipata. Kijiji kilipokea kwa style gani? Hapa ndio tutaita "Kuingizwa kijijini?" 😀 😀

Mkuu Joanah nimefanikisha, tuanze na experience yako:SMILERS:
 
Hahahah mkuu uko fast

Mara ya kwanza kwenda mkoa fulani
Nakumbuka nilifika mchana,kwanza ni namna watu wa ule mkoa walivyokuwa wananiangalia sana,mwanzo sikujua ni nini lakini baadae nilikuja kujua ni namna nilivyokuwa nimevaa

Kilichonishangaza ni lile vumbi,baridi na mvua za karibia kila siku
Suala la usafiri unapanda kiboss tu,sio kukimbizana kama baadhi ya sehemu Dar
Hakuna foleni
Watu wa ule mkoa wanasalimiana asee
Ukiwa na 2k ule mkoa unasurvive hata wiki kwa chakula
Watu wa kule wanakwambia kabisa ile nyumba kuna mama fulani ni mchawi
Wanazika nje ya nyumba tu hapo,yani nje ya nyumba kukuta makaburi mawili matatu ni kawaida kwao 🤦‍♀️
Kingine wanategemea kila mtu anayeishi kule ni wa kabila lao,ukikutana nao wanakuongelesha lugha wanayojua wao

Ms eyes
 
Niko fasta kama umeme 🤣 🤣 ... nawaza kwa jinsi gharama za maisha zilivyopanda kama bado maisha yatakuwa nafuu huko.... suala la kuzikia nje ya njumba hapo kipengele
 
Noumaa sana..
Nilifika kijijini niliambiwa nenda kachunge mbuzi na malosho yalikuwa mitaa chache toka kwa babu.
Basi mimi na udaslamu wangu pamoja na utoto nilikuwa najua kuchunga ni kuchapa/kutembezea makora wale mbuzi, nikajiandaa na fimbo zangu za kutosha kufika malishoni nilichapa mbuzi balaa.

Kasheshe zile mbuzi zilikimbia na kutawanyika kwenye mashamba ya watu hapo nilichanganyikiwa na kushindwa kuzirudiaha pamoja ikabidi nirudi home kuomba msaada.
 
Niko fasta kama umeme 🤣 🤣 ... nawaza kwa jinsi gharama za maisha zilivyopanda kama bado maisha yatakuwa nafuu huko.... suala la kuzikia nje ya njumba hapo kipengele

Nafikiri hayatakuwa magumu sana kama ya hapa Dar kwasababu sio muda mrefu sana tangu nipite huo mkoa

Kaburi zao zipo kila mahali 😂
 
Back
Top Bottom