Uchaguzi 2020 Tulipanda Treni yake, sasa tutapanda Boti, Gwajima achaguliwe

Uchaguzi 2020 Tulipanda Treni yake, sasa tutapanda Boti, Gwajima achaguliwe

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
TULIPANDA TRENI YAKE, SASA TUTAPANDA BOAT. TUTAMCHAGUA

Na, Robert Heriel

Mara yangu ta kwanza kupanda Treni ilikuwa kipindi natoka Mwenge naelekea Bunju B, nikienda kumsalimia Mjomba huko Mabwepande. Sikuwahi kufikiri kuwa Usafiri wa Treni ni mzuri kiasi kile. Nilipouliza ile Treni ni ya Nani, nikajibiwa ni Treni ya Askofu Gwajima, aliinunua. Nilimongeza kimoyo moyo, nikisema; huyu ndiye mtumishi wa Mungu.

Sasa, Askofu Gwajima anaomba kura za wana Kawe. Nawaomba wana Kawe mumchague, Mpeni kura zote za ndio.

Wote tuliopanda Treni yako tutakuchagua Ndugu Mgombea. Wote tuliopata huduma ya pipi ndani ya Treni yako tutakuchagua.

Wana Kawe kuanzia Lugalo, Mbezi Beach, Kunduchi, Tegeta, Mbweni, Boko, Bunju, na Mabwepande wote tutakuunga Mkono.

Gwajima anamoyo wa kutoa sana, hatuna cha kumlipa zaidi ya kumpa kura zetu za ndio.

Tutakuchagua Gwajima
Tutakupigia Kampeni
Tutahakikisha unapata kura zote.

Kama kuna mwana Kawe ambaye hajapanda Treni yako, anyoshe mikono juu, huyo anahaki ya kutokukuchagua. Kama kuna mwana Kawe ambaye hapata huduma ya Pipi kwenye Treni yako huyo asikuchague. Lakini sisi Tutakuchagua.

Hima tukamchague aliyetuletea Treni kutoka Mwenge Mpaka Bunju B.

Baada ya kutimiza ahadi ya Treni na wote tunaiona na tumeipanda. Sasa katuahidi endapo tukimchagua atafanya makubwa zaidi. Atanunua Boat za kisasa za uvuvi, si mnajua Jimbo letu la Kawe limepakana na Bahari ya Hindi, tutavua mpaka tukome, Piga kelele kwa Gwajimaaa! Woyooo!

Kama aliweza kununua Treni na sasa inafanya kazi na tunapanda kila siku kutoka Mwenge mpaka Bunju, kwa nini tusimuamini kuwa atanunua Boat, kisha atanunua Ambulance, woyooo!

Gwajima ni msema kweli
Kawe inamfahamu
Kawe itamchagua

Kawe ya Treni, Kawe ya Boat, Kawe ya Uvuvi, Kawe ya AMbulance.

Hima tumchague mtimiza ahadi.

Maboss wangu wa KAWE, Wazee wangu wa KAWE, Wamama wa kawe, Vijana wa Kawe. Tumchague Gwajima.
Ila Kama hukuwahi kupanda Treni yake, wala hujawahi kuiona basi usimchague.

Yapendeza Treni Yake, Yang'aa Boat zake.

Mtumie mwana Kawe yeyote unayemfahamu ujumbe huu, ili Gwajima apate kura zote.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Back
Top Bottom