Nakubaliana nawe. Ila ukweli ni kuwa uwezekano wa kutokea vita na jirani zetu ni mdogo sana hata kwa miaka 100 ijayo. Binafsi naamini jeshi letu linaweza kuwa standby muda wote na wakati huohuo kutusaidia sana katika kilimo na hata kwenye masuala ya ICT kama tukiamua kuwatumia wanajeshi wetu ipasavyo na kuwapatia mafunzo maalum.
Ndugu yangu sijui unatoa hoja hii kwa uelewa gani ulio nao kuhusu masuala ya ulinzi wa nchi. Nakuona wewe ni mtanzania/mwafrika halisi ambao kawaida yao huwa wanafikiria leo, ya kesho mungu atajua.
Katika sheria za ulinzi wa nchi yaani jeshi la ulinzi la nchi, hakuna muda ambao wako idle, they are on guard every hour, every minute and every second. Issue kama za uzalishaji wa vitu mbali mbali kama chakula na vitu vingine ktk viwanda, hilo linaweza kufanywa na na kuna kuwepo na units for that purpose.
Kwa Tanzania ktk JWTZ tuna idara za ujenzi wa barabara, nyumba n.k. ingawaje ni idara ya ujenzi wanyumba ndo angalau inatumika. Lakini ukweli ni kwamba huwezi kusema eti hatutarajii kuwa na vita kwani majirani wametulia.
Nikikuuliza, mgogoro wa wafanya biashara wa tanzania waliokwama malawi, unajua wanaweza wakapelekea nchi husika zikawa ktk mgogoro? Je, unajua kagame, mseven leo wanawaza nini juu ya TZ?
Unafahamu ni nani amesaidia hicho kikundi cha UN-DRC kupata baadhi ya taarifa juu ya issues za silaha kwenda kwa FDLR?
Ndugu, JWTZ pamoja na kufikiria kujishughulisha na shughuli zingine za uzalishaji mali lazima wawe tayari kwa mazoezi ya kivita kila mara kwani hujui adui atatokea wapi na lini.
Kwanza hata hatuhitaji kuwa bebesha mizigo isiyo yao wanajeshi wetu, tatizo la Tanzania kukosa chakula kila mwaka ni kuwa na watawa (mawaziri) bomu na ufisadi uliokithiri. Pesa yote ya kilimo inaiishia kwenye mikutano, semina, safari, chai, na matumizi binafsi ya watawala.