kaka hata ulaya hutokea hizi ila sisi watanzania hata game za majuu tunazoziangalia tunaangalia magoli na makosa ya refa,..
mfano Robo fainali ya Europe kati ya Liverpool vs Dortmund (Anfield) magoli mawili aliyofungwa Liverpool la 2 & 3 unaweza mlaumu beki ila sio kosa lake,..mpira umepigwa kiufundi na makadirio kiasi kwamba ukizidi uwezo wako wa kuufikia kinatokea (Hamstring),...
sasa weje kuujua mpira hivi vitu vipo je,sisi tunaoufahamu kwa kuanza kuucheza ukubwani itashindika haya kutokea,...
SAFARI YETU KISOKA NI NDEFU ANGALU KUFIKA KAMA SUDAN
mpira ni mchezo wa makosa. taifa stars inaposhindwa wanashindwa wachezaji wote na inaposhinda wanashinda wachezaji wote pamoja na benchi lote la ufundi. haji mwinyi alifanya makosa ya kiuchezaji lakini hatakiwi kulaumiwa kwa sababu wenzake walikuwa wapi kufuta hayo makosa? je na fowadi mbona hawakufunga magoli mengi zaidi ya hayo 2 ya wamisri? je benchi la ufundi kwa nini halikuona mapema kuwa kwa siku ile haji mwinyi hakuwa na utimamu wa mwili tokea mwanzo kutokana na kutoka kwenye majeruhi? mbona samata kakosa penati muhimu wakati timu ilipokuwa inahitaji bao ili kuamsha ari? Kwa hiyo timu team work spirit ni muhimu wameshindwa wote kama timu na hata wangeshinda ni timu nzima ingekuwa imeshinda sio mchezaji mmoja mmoja kama tunavyotaka kuaminishwa hapa. tusiendelee kuingiza ushabiki wa simba na yanga kwenye timu ya taifa kwani itaendelea kutugharimu na kuwakatisha tamaa wachezaji wetu.