Mada haijasema Yanga ni bora, bali inakumbusha tu kuwa timu ikiwa inamuimba Ajib kama ni mkombozi wao, ujue hiyo timu imefilisika. Hili lipo wazi mbona, Yanga ilipomuona Ajib kama mkombozi, Yanga ilikuwa mbovu kiasi kwamba Ajib ndio tegemeo lao.
Simba ilipokuwa bora, Ajib alikuwa hana nafasi kabisa kwenye timu ya Simba kwasababu kuna wachezaji walikuwa wanakiwasha zaidi yake ila leo Ajib kwenye Simba hii ndio anaonekana mtu haswa. Je kiwango chake kimekuwa zaidi ya misimu ya nyuma alipokuwa Simba? Au ndio yeye kwenye orodha ya vilaza wa Simba, ndiye mchezaji mwenye unafuu?