Tuliwaambia Simba imepita njia Nyepesi kufika makundi Cafcl, Wakabisha, Sasa ni vilio Tupu

babu onyango

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2023
Posts
378
Reaction score
984
Tulijaribu kuwaeleza Hawa ndugu zetu kuwa endapo timu hii ingekutana na timu za maana ile hatua ya awali basi hata caf confederation cup isingekuwepo.

Bahati mbaya wakajiona Wana timu ya maana baada ya kuzifunga timu mbovu za de Agosto na Nyasa big bullet.

Sasahivi ni mwendo wa vichapo tu iwe ni taifa au ugenini pote wanapigwa tu.

Hii timu irudishwe kwa Mzee kilomoni tu tujue Moja[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakati ule Simba Sc ilikuwa kwenye form na hapakuwepo hayo mafigisu ya baada ya uchaguzi, kwa ile form ya wakati ule hata Horoya asingetoka salama pale kwake.
Simba bana kwa kujifariji tu hamjambo[emoji1] badala mtengeneze timu yenye class nyie mnategemea form[emoji848][emoji848] kumbuka form ni temporary
 
Wakati ule Simba Sc ilikuwa kwenye form na hapakuwepo hayo mafigisu ya baada ya uchaguzi, kwa ile form ya wakati ule hata Horoya asingetoka salama pale kwake.
Simba ijifunze madhara ya Uchaguzi. Huwezi kufanya Uchaguzi katikati ya ligi wakati Uchaguzi unatengeneza makundi. Yaani CCM wafanye Uchaguzi wa ndani March 2025 halafu Oktoba ufanyike Uchaguzi Mkuu?
 
Tulijaribu kuwaeleza Hawa ndugu zetu kuwa endapo timu hii ingekutana na timu za maana ile hatua ya awali basi hata caf confederation cup isingekuwepo.
Kumbuka hii ni Champions League, sio Shirikisho. Mwezi wa nane kuna Super League, sio Champions League wala Shirikisho. unapoilinganisha Simba ulinganishe na mashindano inayoshiriki, sawa bwana mdogo?
 
Shirikisho lenyewe liliwatoa kamasi mpaka mkaenda kuchoma uwanja wa watu moto ili mpate ushindi lakini wapi mkaambulia kichapo na faini juu ya uchawi wa hadharani sasa unapata wapi mamlaka ya kujimwambafai kuwa unacheza champions league????
 
Muulize pia anacheza champion league yeye ni champion wa nini?
 
Wakati ule Simba Sc ilikuwa kwenye form na hapakuwepo hayo mafigisu ya baada ya uchaguzi, kwa ile form ya wakati ule hata Horoya asingetoka salama pale kwake.
Mkuu Ile game ya horoya tulishamshika kabisa zile nafasi mbili straika mzur anakuachaje pale??? Na mtu akifungwa nyumbani Huwa anapanic mwisho anapigwa nyingi Zaid
 
Simba ijifunze madhara ya Uchaguzi. Huwezi kufanya Uchaguzi katikati ya ligi wakati Uchaguzi unatengeneza makundi. Yaani CCM wafanye Uchaguzi wa ndani March 2025 halafu Oktoba ufanyike Uchaguzi Mkuu?
Hiyo nao sababu? Na endapo Ukifanyika uchaguzi baada ya ligi kuisha na Simba akakosa ubingwa kama ilivyo, makundi hayatakuwepo?
 
Simba ijifunze madhara ya Uchaguzi. Huwezi kufanya Uchaguzi katikati ya ligi wakati Uchaguzi unatengeneza makundi. Yaani CCM wafanye Uchaguzi wa ndani March 2025 halafu Oktoba ufanyike Uchaguzi Mkuu?
Tatizo sio makundi simba shida ni mfumo wa kocha umevuruga team.
Kocha anataka long press simba imezoea pira biliani.
 
Iko hivi kombe la shirikisho ni timu zilizoshindwa. Ni sawa uwachukue wanafunzi waliopata zero Tz nzima uwashindanishe,lazima kuna jinga litakalo PATA div 4 ya 31 halafu litajisifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…