Uchaguzi 2020 Tuliwaambia upinzani ni imani, mkabisha. Kiko wapi?

Kwenye biashara ya CCM ya kununua wapinzani, imekuwa ya hasara kwa wanunuzi na walionunuliwa. Biashara hiyo imewanufaisha zaidi CHADEMA na kupeleka hasara kubwa kwa CCM.

CHADEMA sasa imebakia na wapinzani halisi, mapandikizi na wachumiatumbo wote wameondoka. Imebakia cream ambayo ni vigumu sana kurubuniwa.

CCM imepoteza pesa
CCM imedanganywa na ikadanganyika kuwa upinzani umekwisha. Wakalegea. Rais Magufuli haonekani kujiandaa kuingia kwenye kampeni za ushindani mkubwa kiasi hiki. Wapinzani bidhaa walimpa imani kuwa kwa kuondoka kwao upinzani, basi upinzani umekwisha. Magufuli amekuwa kama amefumaniwa. Hata kwenye kampeni anashindwa kuongea kitu chochote cha maana cha kuwavuta wapiga kura. Amelazimika kubadilisha mikutano ya kampeni na kuwa matamasha ya muziki.

Walionunuliwa, walitegemea faida mbili. Moja kupata fedha na ya pili kupata ubunge au vyeo vingine vitakavyowapa uhakika wa kuendelea kushibisha matumbo yao. Cha ajabu, walio wengi wamenyimwa hata nafasi ya kuwa wagombea. Wachache sana waliopata nafasi ya kuwa wagombea, uwezekano wa kuchaguliwa ni finyu sana. Hawa baada ya uchaguzi watasahaulika jumla.
 
Subiri tar 28 ndo uje ukomenti hapa! Haya mnayoita mafuriko ni marudio tu, tulisha yashuhudia kwa Mrema, Slaa, funga kazi Edo, hadi tulideki barabara! Yaani lisu hapatati hata 10% ya kura! Msije mkaanza kulia lia bure!

Mwaka huu hakuna wizi wa kura... Tume ikichakachua matokeo hapo ndio mwanzo wa vurugu na damu kumwagika...

Kwa taarifa yako nimekutana na baadhi ya polisi nao wapo upande wa TAL..
 
Subiri tar 28 ndo uje ukomenti hapa! Haya mnayoita mafuriko ni marudio tu, tulisha yashuhudia kwa Mrema, Slaa, funga kazi Edo, hadi tulideki barabara! Yaani lisu hapatati hata 10% ya kura! Msije mkaanza kulia lia bure!
Nilifikiri kupitia mafuriko ya hao uliowataja hapo, ungejua kuwa ccm ilishachokwa tangu zamani, ila ni kwa mbeleko ya dola + tume ndo maana wako hapo walipo.
Kwa akili zako hizo nahisi naww ni miongoni mwa washauri wa "hovyo hovyo" wa jiwe lenu.
Vuneni mlichopanda sasa.
 
Kazi na matendo ya CCM ni "the devil himself" sasa sasa sasa (in the tone of sound of the president in line and being electedTAL) tumkatae "one eye devil" kwa matendo yake yote, na kazi zake zote, na hila zake zote. Akwende kureee.
 
Ndugu tuwe wakweli hivi jiwe unaweza mpenda kwa sifa gani kwa mfano?
Mtu ambaye mpaka mke wake anampinga [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Katiba mpya kwao ni mwiba mchungu sana mana wanajua watakuwa wamejichimbia kaburi wenyewe.
 
Vitambulisho vya machinga kaa la Moto?! How?!
 
Kwani Chadema ina wanachama hai wangapi?. Sio kila mass ni wapiga kura wenu, wananchi wengi huja kumwona Lissu wa Ubelgiji ila mioyoni wana yao.
 
Bunge na ccm walishindwaje kuinyoshea kidole serikali kuhusu swala la nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma?
 
Kwamba unataka kusema waliokuwa wanamuaminisha mr haambiliki kafanya wonders Sana kuliko yeyote huko past na staha na level zake ni kuwa kiongozi mkuu wa malaika walimpotosha? Kwamba mtukufu jiwe mtu wa watu msema kweli kipenzi wa Mungu πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† kwamba haihitaji kampeni maana viwonders vyake vinatosha kujiuza.
Jiwe Kama akibahatika kupenya afukuze hao wote vinginevyo akiponyoka saizi atazikwa na ccm 2025
 
Haamini anachokiona!! Leo amepewa tena assignment kama kweli hivyo vitambulisho vya machinga sio vya lazima, basi aifute sheria iliyovianzisha ya waziri wa fedha!!! Sasa atajibu mangapi??
Huwa nawaambia watu kwenye vijiwe huu ni wizi Kama wizi mwingine.Kila mwaka sheria za bajeti na kodi zinaweka ukomo wa mapato yasiyotakiwa kulipiwa kodi,hapo wamachinga wote wanaangukia humo Kama ni kuwatambua haihitaji kutozwa pesa
 
Watu wamepiga hela, watoto wa mjini wamemuingiza chaka Mtupoli.
MaCCM hovyo sana.
Hoja za kuwanyoosha maccm ziko kibao ,kwa mfano miaka yote toka 2016 kila mwaka ripoti za CAG zinaonyesha uozo Sana kwenye serikali na taasisi zake sasa ufisadi na matumizi mabaya ya pesa na upotevu wanaodai kuudhibiti ccm ni upi? Yale mafisadi papa yote yamerudi nyumbani kumenoga yalikozaliwa,kulewa na kuapushwa
 
Nimeamini kila mbabe na mbabe wake.
Magufuli kwa Lissu amelegea, amekua kama gari ya mkaa tripu shamba, tripu gereji. Mtupoli karudi dodoma alipoanzia.
Achana na LISSU kabisa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…