Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kwenye biashara ya CCM ya kununua wapinzani, imekuwa ya hasara kwa wanunuzi na walionunuliwa. Biashara hiyo imewanufaisha zaidi CHADEMA na kupeleka hasara kubwa kwa CCM.
CHADEMA sasa imebakia na wapinzani halisi, mapandikizi na wachumiatumbo wote wameondoka. Imebakia cream ambayo ni vigumu sana kurubuniwa.
CCM imepoteza pesa
CCM imedanganywa na ikadanganyika kuwa upinzani umekwisha. Wakalegea. Rais Magufuli haonekani kujiandaa kuingia kwenye kampeni za ushindani mkubwa kiasi hiki. Wapinzani bidhaa walimpa imani kuwa kwa kuondoka kwao upinzani, basi upinzani umekwisha. Magufuli amekuwa kama amefumaniwa. Hata kwenye kampeni anashindwa kuongea kitu chochote cha maana cha kuwavuta wapiga kura. Amelazimika kubadilisha mikutano ya kampeni na kuwa matamasha ya muziki.
Walionunuliwa, walitegemea faida mbili. Moja kupata fedha na ya pili kupata ubunge au vyeo vingine vitakavyowapa uhakika wa kuendelea kushibisha matumbo yao. Cha ajabu, walio wengi wamenyimwa hata nafasi ya kuwa wagombea. Wachache sana waliopata nafasi ya kuwa wagombea, uwezekano wa kuchaguliwa ni finyu sana. Hawa baada ya uchaguzi watasahaulika jumla.