Tuliyemtarajia atamfunga paka kengele, kaamua kukaa pembeni

Tuliyemtarajia atamfunga paka kengele, kaamua kukaa pembeni

MWANAHARAMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
5,350
Reaction score
13,622
Tuliyemtarajia atamfunga paka kengele, kaamua kukaa pembeni
Huyu alifikiriwa ataleta Imani, tumaini na hali mpya ya kupoza joto linalo panda kati ya Shume na panya wa mwituni.

Sasa kaamua kushuka, wenyewe wanasema katelemka ngazi,
haelewi uelekeo wa chombo,
hajui kama kinazama au kipo njia sahihi.

Panya wanajiuliza, wafanyeje
Maana pakashume anazidi kuleta, vishume vidogo dogo kwenye Kila Nyanza ya pori

Pori si salama tena
Mkombozi yupo Lupango
Aliyetarajiwa Kutoka upakani
Naye kaona kina kirefu
Panya wapo kizani.

Nini panya wafanye ili
Waweze kujikomboa
Kabla janga la mgawanyo
Wa Imani halijachukua tamati
 
Inaonekana mpaka sasa Pashume ameshindikana! hadhibitiki.
 
Back
Top Bottom