Tulizoea maisha ya ujanja ujanja kurudi kwenye halali tunaona nongwa

Tulizoea maisha ya ujanja ujanja kurudi kwenye halali tunaona nongwa

Akili nyingine sijui hata mmeziokota au ndio hizi za kuzaliwa nazo?
Hakuna mtu anapinga kulipa kodi enyi wapumbavu , kinachopingwa ni utaratibu mbaya na mazingira ya hizo kodi zenu. Umeua biashara, umeshindwa kutengeneza mazingira rafiki, umeshindwa hata kuvutia wawekezaji halafu unabwabwaja eti watu walipe kodi, na wakishalipa kodi hela zao unazifanyia nini ambacho kitawanufaisha walipa kodi kama sio kuzitumia kwenye chaguzi za kijinga.
Mnatumwa kuja kuandika tu bila hata kuwahoji wanaowatuma.
Hapo ndo kwenye utata kodi hazitumiki ipasavyo kwenye maendeleo
 
Kodi kila mtu anataka kulipa, vile vile tunahitaji mazingira mazuri ya kufanyia biashara. HAKUNA NCHI DUNIA HII ILIYOENDELEA KWA KUWAFANYA MATAJIRI WAISHI KIMASIKINI.
Kama utajiriwako ulikua wa kukwepa kodi ni kweli utarudi kuwa maskini.
 
Hakuna nchi dunia hii itaendeshwa bila kodi.lazima tukamuliwe ili hela ipatikane tuache kupewa mikopo ya masharti ya kipumbavu.
Kodi unanunulia wapinzani alafu unajitapa eti nchi ni tajiri......fyoko
 
Kung'ang'ania kodi zilipwe wakati unaua uchumi na biashara ni sawa na kutarajia coaster ikuingizie pesa kila siku ila gereji huipeleki ipo siku Engine ita noki tu na ndio utakuwa mwisho wa mchezo!

We need proper money distribution as well as stable markets ili biashara ziende vyema, watu watalipa kodi tu tena bila kutumia nguvu! Ila kwa sasa wacha watu wahamie instagram na kupanga vimeza road maana kufungua fremu tu nongwa!
Hakuna biashara za magumashi kipindi hiki.
 
Akili nyingine sijui hata mmeziokota au ndio hizi za kuzaliwa nazo?
Hakuna mtu anapinga kulipa kodi enyi wapumbavu , kinachopingwa ni utaratibu mbaya na mazingira ya hizo kodi zenu. Umeua biashara, umeshindwa kutengeneza mazingira rafiki, umeshindwa hata kuvutia wawekezaji halafu unabwabwaja eti watu walipe kodi, na wakishalipa kodi hela zao unazifanyia nini ambacho kitawanufaisha walipa kodi kama sio kuzitumia kwenye chaguzi za kijinga.
Mnatumwa kuja kuandika tu bila hata kuwahoji wanaowatuma.
Akuna anaye tumwa sisi ni watanzania na tulikua tukiyaona yanayotokea. Hakuna anaye wachukia wafanya biashara tatizo lipo kwa wale waliokua wanafanya nchi hii shamba la bibi.
 
Akuna anaye tumwa sisi ni watanzania na tulikua tukiyaona yanayotokea. Hakuna anaye wachukia wafanya biashara tatizo lipo kwa wale waliokua wanafanya nchi hii shamba la bibi.
Hao kina sijui nani hamuwajui? Hapa hatupigi story sijui za nani mwizi na kama mnawajua mahakama si mmeanzisha mnashindwa nini kuwakamata?
Tunachosema hapa ni utaratibu mzuri na matumizi mazuri ya hizo kodi na sio kuhitaji kukusanya tu bila kuweka utaratibu mzuri unaomsaidia mtoa kodi.
Kwa kutotaka kujua hata ile ndogo tu mtaikosa kwa ubishi wenu.
 
Kwa taarifa yako biashara kwa Sasa ndio zimeshamiri.watu wengi yu tunawajua wanapiga hela kwenye biashara.na kwanini useme utaratibu mbaya.fafanua vizuri kipi kimekosewa
Nyie kula kulala, tupe mifano ya hao wafanya biashara wanao piha pesa ndefu.
 
Back
Top Bottom