Tumaini Nyamhoka (Rais TUCTA) wafanyakazi wa wapi walikutuma ukaseme hawataki nyongeza ya mshahara mwaka huu?

Tumaini Nyamhoka (Rais TUCTA) wafanyakazi wa wapi walikutuma ukaseme hawataki nyongeza ya mshahara mwaka huu?

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,898
Reaction score
40,547
Akihutubia wafanyakazi waliojitokeza kwenye kilele cha sherehe za Siku ya wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2026) Rais Samia amesema mwaka huu TUCTA hawakwenda na madai ya mshahara mpya na viongozi wao walimwambia Rais "mwaka Jana ulikuwa na kazi nzito ya uchaguzi na pia miundombinu imeharibiwa na Machafuko ya Oct 29, 2025 pamoja na mvua za masika, hivyo hatukudai labda mwakaniii".

Swali langu kwa Rais wa TUCTA ni Watumishi wa Kada gani walikwambia maneno hayo ukamwambie Rais? Kwa hiyo fedha za nyongeza ya mishahara ya Watumishi ni sahihi igharamie uchaguzi wa kisiasa? Kwamba Watumishi wa nchi hii wanapenda Sana siasa kiasi cha kuwa tayari Ku-sacrifice nyongeza yao ya mishahara ili Madiwani na wabunge wakale perdiem?

Au ni Uchawa wako tu ila Rais kakuumbua hukutegemea kama anasema pale?
 
Hiv Zanzibar hakuna TUCTA??

Mbona kula wafanyakazi wamekumbukwa.?
 
Back
Top Bottom