Dear tough lady,
kwanza pole sana , maana inaonekana Tumain wamekubore sana, mimi kama mmoja wa wanafunzi waliomaliza Tumaini University Dar - ningependa kukushauri yafuatayo .TCU inaruhusu mwanafunzi kuhama chuo kimoja kwenda kingine, ninauhakika kabisa ukiomba uhamisho utaruhusiwa kuhamia University yeyote hapa Tanzania na utamalizia masomo yako kwa amani na furaha - "Why dont you do that?", pamoja na matatizo yote hayo yaliyopo sidhani kama unakitendea haki chuo kwa kuonyesha kila kitu pale Tumaini ni kibovu sana- jambo hilo sio kweli, mfano umezungumzia swala la walimu kukosekana kwa nusu ya semester na ukatolea mfano wa BA education,je hili ni tatizo la kila semester?au ilikuwa only once?,Tumaini kuna degree zaidi ya moja, je umewahi kusikia wanafunzi wa BBA, BHRM , BALIS OR BIM? wanalalamika kwa kukosa walimu?, huwatendei haki wanafunzi wenzako kwasababu unaonyesha kuwa hawafundishwi iipasavyo hivyo degree yao ni "half cooked". Je mtu akikataa kuwaajili wanafunzi wa tudarco wa BBA, BIM, BALIS OR BHRM kwasababu uliutangazia umma kuwa hawafundishwi itakuwa sahihi?. Please don't generalize the issue. Pia umezungumzia madarasa kuwa godown, its true, but hali sio mbaya kivile kamaunavyotaka jamii iamini, uzuri umesema utaweka picha, please ukiweka picha weka zote ya nje na ndani pia, ili wadau wapate kuona na kuchangia.Mimi nafikiri tatizo lako wala sio madarasa wala walimu ni hela ya field. Kwasababu kama ni madarasa toka siku ya yako kwanza pale chuoni uliyaona na still ukaamua kubaki kwasababu ungeweza kuhama chuo.Hata swala lako la pesa za field am sure kutakuwa na maelezo ya kuridhisha why zimechelewa , ushauri wangu piga simu au nenda utapata uhakika wa nini kinaendelea, tena unaweza ukaongea na hata mkuu wa chuo hakuna atakaye kuzuia. kuna watu wengi tu wameajiliwa sehemu mbalimbali na wana position nzuri tu, kwa kutumia cheti hicho hicho cha Tudarco-ambayo wewe unasema haifai kabisa na wanaperform vizuri sana kuliko hata waliosoma udsm or mzumbe.Nisingependa kuandika sanaaa, but malalamiko yako yote yana majibu ya kuridhisha am sure, tatizo ni moja, unatafuta majibu sehemu sio sahihi.Nawakilisha.