Mwizukulu mgikuru
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 6,788
- 16,227
kwamba nina miaka 40 sina gari wala nyumba lakini leo chuo kikuu cha mzumbe nimehitimu shahada yangu ya tatu na kutunukiwa PHD....je haya sio mafanikio?.... nina umri wa miaka 40 nimeowa na nina watoto watatu wa kwanza kamaliza shahada ya udaktari kcmc moshi na wa mwisho anachukua kozi ya uuguzi chuo cha tandabu jijini mwanza. je haya sio mafanikio 😊😊 Nina umri wa miaka 40 sina nyumba sina gari ...nimejiajili, mimi ni dalali , nimepanga chumba na sebule jijini daressalam ninaishi masaki, ninau hakika wa kula vizuri na kuvaa vizuri na hata kuwasaidia chochote ndugu na jamaa je haya sio mafanikio? 😊😊 Ninayo mifano mingi lakini kwa leo niishie hapa hebu tujadili mafanikio..