tumalize mjadala leo...mafanikio ni kumiliki gari na nyumba?😊😊

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
6,788
Reaction score
16,227
kwamba nina miaka 40 sina gari wala nyumba lakini leo chuo kikuu cha mzumbe nimehitimu shahada yangu ya tatu na kutunukiwa PHD....je haya sio mafanikio?.... nina umri wa miaka 40 nimeowa na nina watoto watatu wa kwanza kamaliza shahada ya udaktari kcmc moshi na wa mwisho anachukua kozi ya uuguzi chuo cha tandabu jijini mwanza. je haya sio mafanikio 😊😊 Nina umri wa miaka 40 sina nyumba sina gari ...nimejiajili, mimi ni dalali , nimepanga chumba na sebule jijini daressalam ninaishi masaki, ninau hakika wa kula vizuri na kuvaa vizuri na hata kuwasaidia chochote ndugu na jamaa je haya sio mafanikio? 😊😊 Ninayo mifano mingi lakini kwa leo niishie hapa hebu tujadili mafanikio..
 
Hata tukijadili leo, huu mjadala hauishi. Watakuja wengine nao watajadili.

Mafanikio ni mtazamo/perspective ya mtu, kwangu kuwa na ghetto lenye samani zote, TV, fridge, kochi la wawili, jiko la gesi, kabati ya nguo ni mafanikio. Kwa mwingine nyumba, gari, mashamba ni mafanikio na kwa mwingine kiwanda, kampuni, biashara kubwa ni mafanikio.
 
Mjadala ufungwe, umeshamaliza kila kitu.
 
Mafanikio ni kutimiza ndoto ulizo jiwekea coz kila mtu ana malengo na vipaumbele tofauti katika maisha,

Mafanikio hayapimwi kwa viwango vya watu wengine au jamii,bali yanapimwa kwa namna unavyo fikia yale malengo unayo yaona yana maana kwako binafsi,iwe katika kazi,afya,familia au maendeleo ya kiroho.
 
Hakika,
Mwingine kulala na poshy queen nayo ni mafanikio kwake
Your browser is not able to display this video.
 
Vyote bado siyo mafanikio hizo ni nyenzo tu za kawaida za kimaisha,itakuwa mafanikio kweli kama mwenye navyo atakuwa na 100% ya kufa akiwa navyo bado.

Mafanikio ya uhakika kwa binadamu anayeishi ni kifo tu,huu ndiyo mchongo wa uhakika tunategemea uta-tick anytime.
 
Kumaliza PhD ni mafanikio pia , kuamka asubuhi ukiwa mzima wa afya ni mafanikio pia , kufika ofisini kwako kutoka nyumbani kwako ni mafanikio pia .

Hayo mengine , mambo ya kujilinganisha tu yaani binadamu tunapenda tufanane..Mimi binafsi sina hobby ya kununua magari kabisa , nyumba sawa ila magari hapana yaani nikiona mtu anapost gari namuona mshamba sana . Usijilingane na mtu , mpaka unapata PhD ni mafanikio makubwa .​
 
Mafanikio ni fullfillment

Kufikia kila unachoona ni goal kubwa zaidi maishani mwako kiasi cha kuridhika na pale ulipo kihisia na kiakili (sio kubweteka)

Sasa ukichambua kwa angle hii utaona kila mtu ana namna yake anavyoyatafsiri mafanikio.

Expectations alizonazo kwenye maisha yake ambayo yanategemea pia background yake, level of exposure and ambition yake. So hakuna mtu wa kufanya conclusion kwa kitu chenye tasiri tofauti kwa watu tofauti
 
Mafanikio ni subjective ina maana kila mtu ana definition yake mwenyewe.

Ukienda Kilosa kuna tajiri anaitwa Babylon lakini akija town anazidiwa hata na Chawa Baba Levo lakini huko kwao ni mtu ambaye wanakilosa wote wanamuona ni TAJIRI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…