tumalize mjadala leo...mafanikio ni kumiliki gari na nyumba?😊😊

Kwanza nakukumbusha kua neno mafanikio yametokana na neno kufanikiwa sasa mafanikio ni ile hali ya kufanikiwa kile ulichopanga binafsi,kikundi,jamii,nchi kiufupi ili kufanikiwa kuwepo lazima kutanguliye malengo (PIA MALENGO HAYAFANANI KWAHIYO MAFANIKIO HAYAFANANI PIA)
 
Yoote hayo ni mafanikio ktk Nyanja tofauti tofauti, tatizo la Watz wanataka mafanikio yafanane
 
Hata uwe umesoma vipi, kama unashindwa kujimudu na kuhudumia familia we ni lofa tu na hiyo elimu haina maana.
 
Bila gari sasa pesa unakua nazo zanini mkuu ,kma pesa ndio utelez wa maisha
 
Kumiliki gari pekee sio mafanikio wala kumiliki nyumba..hayo NI mahitaji muhimu ya mwanadamu Kwa Karne ya SASA.

Ila aina ya gari unalomiliki au aina ya nyumba unayoishi au kumiliki vinaweza kuwa mafanikio Kwa pamoja na milestones mbalimbali Katika maisha yako
 
Inategemeana mafanikio ni kutimiza ndoto zako ,na pia mafanikio namna nyingine kumiliki mali nyumba ,biashara ,gari ,nyumba nk
 
Mimi mafanikio yangu niijiwekea kumiliki kadigrii ka uhandisi lakini leo sina chapa mia mbovu ila karoho baridi hata nikifa nakuwa mfu msomi inatosha kabisa niende nikafanye ma calculus na Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…