SoC01 Tumalize Tatizo la udini Tanzania "Mungu siyo mzungu"

SoC01 Tumalize Tatizo la udini Tanzania "Mungu siyo mzungu"

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Sep 15, 2015
Posts
57
Reaction score
31
Udini ni tatizo ambalo lipo sana kwenye jamii yetu ya Tanzania na linatutafuna. Hatuna vita vya mapanga na risasi lakini kisaikolojia tuna vita kubwa sana! Nimeshududia mitafaruku katika ndoa,koo fulani,familia kuvunjika na hata sometimes kuligawa taifa letu hasa wakati huu wa korona.Hii yote ni kutokana na uelewa duni wa imani na mambo ya kimungu.
nielezee neno mungu ili tuelewane kabla:

Mungu!
Mungu ni nguvu ya juu zaidi na kubwa ya asili ambayo chanzo cha kila kitu katika ulimwengu(universe).

Kwa lugha ya kigeni God is a super-natural power acting in a universe! Nguvu hii ndiyo inayo-control dunia kwa misingi asilia ya ulimwengu! Tofauti na watanzania wengi wanavyodhani ni kiumbe hai kama alivyo binadamu au taswira wanazojenga vichwani mwao.Nguvu hii ipo connected na kila kitu kilichopo ndani ya ulimwengu iwe binadamu, mnyama, miti au material things! Nguvu ya misingi ambayo haibadiliki lazima uifuate vinginevyo itakutoa ulimwenguni(kufa/dis-appear) lakini unaweza kuitumia pia.

Chimbuko la tatizo
Jinsi ya ku-activate nguvu hizi ndiyo tatizo linapoanzia..! kumbuka kuwa Binadamu pia tupo connected na nguvu hizi za mazingira( God is nature in other words).Hapa ndiyo tunapata dini mbalimbali lakini wote tukitafuta nguvu ile ile ambaye ni mungu kama utangulizi ili kuenenda na misingi ya ulimwengu ambayo lazima tuifuate! Duniani kuna dini/ njia nyingi lakini nitaongelea nchi yangu Tanzania tu kwa leo!
Kwa Tanzania tuna njia tatu

1:kutambika/ Traditional religions
Hii pia ni njia ya ku-activate nguvu asili( kumfikia mungu) kwa kutambika! Nguvu/Mungu ambaye huyo huyo anatafutwa na waislamu na wakristo.kuna ibada zinafanyika na mafanikio makubwa watu wamepata kutokana na njia hii.wengi wameishi duniani kwa amani sana na miaka mingi ya kutosha kwa kuweka imani zao katika dini hii.Nitakuja kuleta mifano dhahili ya hii dini

2: wakristo
Hii ni imani/dini kubwa tanzania ambao nao wana-activate nguvu asilia( kumtafuta mungu) kwa jina/damu ya yesu(yesu ni daraja la kuactivate hizo nguvu/kumuona mungu).pia hawa wana mafanikio makubwa cha msingi kufuata vigezo na masharti ya njia hii(biblia).


3:waislamu
Hii pia ni dini kubwa hapa Tanzania ambao nao wana-activate nguvu asilia(kumtafuta mwenyezi mungu) kupitia mtume mohamad ambae pia ni daraja.vile vile watu wamefanikiwa sana lakini vigezo na masharti vizingatiwe(Quaran).

Zingatia:
a) Njia zote zipo sahihi kabisa kuzifuata na zitakupa mafanikio na mwisho mzuri cha msingi vigezo na masharti vizingatiwe( misingi ya ulimwengu)

b) Usidharau imani(njia) ya mwingine! Mwenye nguvu kati yenu ni yule aliyesimama imara katika imani yake

C) Imani zote zina nguvu sawa kinachotutofautisha ni nguvu/uthabiti baina ya mtu na mtu katika Imani yake.

d) binadamu wote ni sawa na tuna daraja moja tu(kifo) isitoshe pua zimeangalia chini. Tuishi vizuri chini ya jua.

PIGA VITA UDINI ILI KUIJENGA TANZANIA
 
Upvote 2
Back
Top Bottom