Hivi wanaosema Sema Chama anakuwa mbaya team ikizidiwa, na mzuri team ikiwa inamiliki mpira, wanawaza nini ? Hivi nichezaji gani anakuwaga bora team ikiwa imezidiwa? Juzi tu Argentina ilifungwa na na Saudia na Messi akiwa ndani.
Tunachoangalia ni overall performance ya mchezaji katika team. Chama ameamua mechi nyingi sana muhimu kwa Simba ukianza ya Nkana, Al alhy, AS Vita na ya juzi ya Horoya. Amekuwa bora siku zote, killer pass nyingi sana, statistics zake za ndani ya ligi yetu na nje kwa maana ya mashindano ya caf yanambeba Chama, So far ndy top scorer kwa hii Champions league. Tatizo mnapenda kujadili mambo kwa ushabiki kuliko uhalisia, na mnajadili bila ya kuwa na takwimu.