Hekari moja hutumia mifuko 5 ya mbolea. NPK 10:18:24 mifuko 4 na CAN 27 mfuko 1.
Heka moja huzalisha kilo wastani wa 560kg hadi 1000 kg kutegemea na matunzo yako shambani ikiwa ni pamoja na kupanda mbegu bora,uwekaji mbolea kwa kuzingatia vipimo sahihi vilivyopendekezwa,palizi kwa wakati,kutifulia vizuri,ukatiaji vikonyo, kudhibiti wadudu waharibifu na muhimu kabisa uvunaji sahihi wa majani yaliyokomaa na uchomaji bora.
Masoko. Madaraja ya bei za tumbaku hapo mengi,zaidi ya madaraja 20. Daraja la juu huitwa L10F ,hili bei yake ktk dola 3.200 USD kushuka hadi daraja 0. Heka moja ukizingatia utunzaji mzuri wa kibongobongo huweza kupata 3.5 nakuendelea. Endapo hutokumbana na majanga ya asili,kama mvua ya mawe,upepo mkali na mvua kupita kiasi kama ya mwaka huu na uwe umelimia kwenye ardhi ya kutuamisha maji,tambua haya ndo majanga pekee. Mchawi pekee wa tumbaku ni matunzo shambani ya wakati na dozi bora ya mbolea.
Picha: Mfano wa karatasi ya bei ya mauzo kwa madaraja ya tumbaku.
L10F, C1L,M10,L30 nk. Tumbaku huuzwa ktk dola tu.