Tumbo halijarudia hali ya kawaida baada ya kujifungua

crome20

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
1,193
Reaction score
810
Hallo Doctors, Nisaidie kujua kama kuna jambo tumelikosea ,au limekosewa na wataalamu kuhusu kutorudia hali ya kawaida ya mke wangu baada ya kujifugua.

Ukweli ni kuwa , ujauzito wa kwanza ulikua bahati mbaya baada ya mtoto kutoka akiwa amechoka sana na walilazimika manesi kumvuta, na kuongeza njia sehemu za siri baada ya njia kuonekana ndogo. Hapo ilikuwa Muhimbili 2000. Ujauzito wa pili na wa tatu alifanyiwa operation Mikocheni Hosp.

Ujauzito wa pili actually mtoto alikuwa na kilo 4.9kg kitu ambacho asingeweza kujifungua kawaida. Wa tatu nadhani history ilitumika zaidi na sasa tumeamua kuishia hapo. Sasa cha ajabu tumbo la mke wangu halijarudia hata very close to normal. Anaonekana kama mjamzito wa 4months hivi kitu amabacho we don't feel comfortable with.

Tunafikiria labda kuna mazoezi ya kusaidia hali hiyo lakini hatujapata ushauri wa kutosha ndo maana nimeingia jamvini mnisaidie jamani. I love her and she look very sexy with slim belly .
 
Ninavyofahamu akishajifungua tu anapaswa afunge kanga/kitenge tumboni ili tumbo lirudie hali yake ya kawaida. Je hilo lilifanyika
 
Ninavyofahamu akishajifungua tu anapaswa afunge kanga/kitenge tumboni ili tumbo lirudie hali yake ya kawaida. Je hilo lilifanyika
No hawezi kufunga kanga wakati amefanyiwa operation, kanga au kitenge hufungwa na mama aliyejifungua kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujifungua. Kwa uzoefu wangu (maana mimi si daktari), mama aliyejifungua kwa operation, anatakiwa asubiri kidonda kipone (sijui ni miezi mingapi) ndipo anaruhusiwa aidha kufanya mazoezi ya tumbo au kuvaa belt tumboni kwa ajili ya kupunguza tumbo hilo. Ila wataalm naomba waeleze kitaalam zaidi(daktari au nesi)
 
Aende kwa wamasai watakuwa na dawa tu kwa hospitali hakuna msaada
 
lilifanyika, but kumbuka anakuwa na scar ya scissor so hawezi kufunga kama mtu wa kawaida. Lakini kwa ile bahati mbaya kanga na kukanda vilifanyika barabara.
Ninavyofahamu akishajifungua tu anapaswa afunge kanga/kitenge tumboni ili tumbo lirudie hali yake ya kawaida. Je hilo lilifanyika
 
Utaweza kumwambia mwanao kuwa "mulimzaa kwa bahati mbaya?"
 
Nenda dynapham wanadawa asili,nipm pia nkpe namba ya dada mmoja anadawa za india znapunguza vtambi! Kngne kbariana na hali mana uzaz una mambo ikiwa pamoja na kupoteza shape kbsa.
 
Utaweza kumwambia mwanao kuwa "mulimzaa kwa bahati mbaya?"

asemapo alikuwa bahati mbaya means it was still birth.

kwa waswahili ndio husema mtoto bahati mbaya ama kapata mtoto bahati mbaya.
 
asemapo alikuwa bahati mbaya means it was still birth.

kwa waswahili ndio husema mtoto bahati mbaya ama kapata mtoto bahati mbaya.

Yeye aliposema "ujauzito wa kwanza ulikua bahati mbaya" ndipo aliponichanganya

Btw: Mimi nimezowea kusikia "tumezaa ila haikuwa rizki", au "mtoto hakuwa riziki" ...hii ya "mtoto bahati mbaya" ndio naisikia leo
 
rudi kwa gny wako ampime isije ikawa mkeo ana fibroids zikawa zinajaza tumbo ndo mana linaonekana kubwa sana.
but kama hana its all about exercise especially seat ups na swimming zitamfanya tumbo linywee.

lakini pia kuna blog moja nimeiona hmu juzi ikitangazwa sijui niipate wapi but niya @suctus mtsimbe inaelezea home remedy za matatizo mbali mbali nafikiri can help you. otherwise nakuibia tu kidogo

chukua limao moja kamua maji yake yaani juisi, tia punje moja ya garllic iliyosagwa na tangawizi kipande kidogo kilichosagwa, weka chumvi iwe kali lakin iweze kunyweka tia maji kidogo ya uvuguvugu yafike kikombe cha chai (siyo mug) basi mpe anywe kila baada ya siku 3 ndo anywe. ataharisha sana hiyo atatoa uchafu wote tumboni plus mafuta mafuta.

while doing it a observe kula thermogenic foods like fruits especially carrots, matango, mboga za majani, jamii ya kunde (maharage njegere etc) chai anywe ya kutumia green tea, iwekwe asali, tangawizi na mdalasini. wanga asile hivyo a suppliment kwa kula mboga matunda na juice zisizo na sukari.

chonde mm sio daktari nimesema tu na sibebi dhamana ya matokeo uyapatayo nanawa mikono.
 
Yeye aliposema "ujauzito wa kwanza ulikua bahati mbaya" ndipo aliponichanganya

Btw: Mimi nimezowea kusikia "tumezaa ila haikuwa rizki", au "mtoto hakuwa riziki" ...hii ya "mtoto bahati mbaya" ndio naisikia leo
dah! uko mbali kweli rafiki siku hizi watu hawasemi hivyo kwasababu mtoto siyo riziki waliitafsiri kwamba ni mtoto wa kiume shoga. so wenye busara zao wakaja na msemo mtoto bahati mbaya.
 
Nimepick some good eating habit, na hiyo ya swimming nimeipenda asante nachukua points kadhaa na kuchukia taadhari hasa hiyo ya kuharisha, nsije nkazalisha mengine. Thanks
 
Kajifungua kwa operation lakini

Ninavyofahamu akishajifungua tu anapaswa afunge kanga/kitenge tumboni ili tumbo lirudie hali yake ya kawaida. Je hilo lilifanyika
 
afanye mazoezi kidogo kidogo
pia angalia na diet yake, asikule sana.
 
crome20, kuna sababu kama 4 za mtu kuwa na tumbo kubwa.

1. Kujifungua kwa akina mama. Wengi tumbo huwa kubwa na kujirudi taratibu. Kimila wengi hukandwa na kujifunga nguo au kanga ya kubana kwa muda fulani. Mara nyingi njia hii ni ya waliojifungua kawaida.

2. Tumbo kujaa gas au kuwa na gesi: hii inatokana na vyakula tunavyokula

3. Tumbo kuwa na mafuta, ndani kabisa ya viungo vya mwili vilivyo ndani ya tumbo. Na hapa kuna vesceral fat ambayo ni killer fat.

4. Mafuta yaliyopo juu ya tumbo.

Katika case yako sina uhakika, ila ni wazi kuwa kama mama alijifungua kwa OPS basi baada ya kutolewa mtoto tumbo la uzazi bado halijarudi. Gyno wako anaweza kukushauri.

Lakini jaribu pia kufanya yafuatayo:

1. Aobserve healthy diet. Atumie chakula chenye low calories but high vitamins: veggies, matunda, roots food nk.

2. Atumie diet ya kupunguza uzito, assumption ni kuwa tumbo lina mafuta. Aanaweza kutumia juice ya limao moja aweke kwenye maji (glass)ya uvuguvugu na vijiko 2 vya asali. Atumie asubuhi akiamka tu na jioni kabla ya kulala. Pia atumie Green tea na aweke asali badala ya sukari kila anapotaka kunywa chai. Hii ina-burn fat very fast.

3. Afanye therapy ya digestive system once kila baada ya siku 3-5: Achanganganye limao 1 (akamue); Kitunguu swaumu kidogo (Apondponde) na Tangawizi (apondeponde) na kuweka katika glass ya maji ya uvuguvugu. Kisha aweke chumvi ya kutosha na kunywa. Hii inaondoa gesi na kuburn fat.

Kwa details: Mafanikio Na Afya Njema
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…