Tumbo Kujaa Gas

Jallen

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Posts
517
Reaction score
196
Naombeni ushauri juu ya tumbo kujaa gas na kutopata choo, nitumie njia gani kuondokana na adha hii?
 
Hili tatizo limenisumbua sana,ila sasa hivi nimepata nafuu sana baada ya kuanza kutumia maji ya moto(uvuguvugu) asubuhi ninapoamka kabla sijala kitu wala kupiga mswaki glass 2,baada ya chai galssi 1,kwakuwa naenda kazini sipati nafasi ya kupata maji ya moto lakini ninaporudi nyumbani nusu saa kabla ya chakula glassi 1 na nusu saa baada ya kula glassi 1,pia asubuhi chai yangu naweka mdalasini sasa sijajua kama nitapona kabisa hii hali au ni kwa muda,ila imenisaidia sana,try it and u can give me feedback.
 
1. Hakikisha unaepuka kula junk food ikiwemo pia vinywaji vilivyosindikwa.
2. Kula sana matunda na vyakula vya kambakamba hususani mboga za majani.
3. Epuka kula vyakula vilivyokobolewa.
4. Kunywa maji mengi kwa siku.
 
Mkuu.@Jallen pole sana kwa kuumwa na gas ukitaka upone fuata Maagizo ya mkuu.@stephot kwa kunywa maji ya Uvuguvugu kila Asubuhi unapoamka kunywa glasi 3 kabla kula kitu na baada ya saa 1 kupita waweza kula

chakula na wakati wa mchana kabla ya kula kitu tumia tena maji ya Uvuguvugu glasi 2 kisha baada ya saa 1 kupita

ndio waweza kula chakula na wakati wa usiku kabla ya kula chakula kunywa maji tena ya uvuguvugu kabla ya

kula kitu usiku glasi moja kisha ukae baada ya saa 1 kupita waweza kula chakula na wakati wa kulala fanya

kunywa glasi 1 ya maji ya uvuguvgu kisha waweza kulala fanya hivyo kila siku utapona hayo matatizo yako

ya kutoweza pata choo. Pia uwe unatumia punje moja ya Kitunguu saumu kitakusaidia kuondosha Gesi

uliyokuwa nayo tumboni na unaweza kutembelea hapa kuona Faida ya Maji ya Uvuguvugu bonyeza hapa
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/365977-muujiza-ya-matibabu-kwa-maji-ya-moto-kunywa.html
 
Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda choo. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.


Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa

‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula

vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.


Chanzo. https://www.jamiiforums.com/jf-doct...ukosa-choo-kwa-muda-mrefu-constipation-4.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…