Tumbua tumbua inayofanywa na mawaziri Jafo na Aweso ni kama vile hawakuwepo kwenye Wizara hizo!

Tumbua tumbua inayofanywa na mawaziri Jafo na Aweso ni kama vile hawakuwepo kwenye Wizara hizo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo siyo mgeni wizarani hapo amekuwepo tokea muhula wa kwanza wa Rais Magufuli kadhalika Waziri wa maji Juma Awesu alikuwa Naibu waziri kwenye wizara hiyo.

Nimefuatilia ziara za mawaziri hawa mikoani na kushuhudia wakipiga mikwara mizito kusimamisha kazi na kutumbua kana kwamba wao ni mawaziri wapya kwenye wizara zao.

Ndio najiuliza ni kutafuta kiki au kukosekana wapinzani ni tatizo?

Maendeleo hayana vyama!
 
Hii awamu ya tano kiongozi bila kutumbua anajiona hajafanya kazi, wamegeuza hicho kitendo kimekuwa cha kawaida kama fasheni, wasiwasi wangu wasiwaonee tu hao wanaowatumbua.
Kuna DED fulani mbabe jijini hapa Dar, waliposikia tu Jafo kabaki Uwaziri, kaugua wiki nzima.
Sijui kwa nini?
 
Watendaji watawakumbuka Chadema maana walikuwa ndio sehemu ya kutafutia kiki hawa mawaziri.

Nadhani hata bunge " litadoda" sana!

Maendeleo hayana vyama!
Huhitaji kusubiri mpaka bunge lianze kujua kuwa litakuwa halina mvuto. Hilo bunge natabiri litakuwa kama uji wa baridi usio na sukari. Wataishia kutunga sheria kandamizi ili kuingia kwenye mijadala ya wananchi, lakini hawatakuwa na jipya. Hayo ndio madhara ya kupata madaraka kisheria bila ridhaa ya umma.
 
Awamu ya Tano ikiisha itatuacha kwenye maumivu makubwa sana ya kiuchumi...Inafanya kazi iwa mihemko ujuaji na kukomoana.
Mbaya zaidi mnafukuza wawekezaji ona sasa Dangote ameshafunga kiwanda.
 
Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo siyo mgeni wizarani hapo amekuwepo tokea muhula wa kwanza wa Rais Magufuli kadhalika Waziri wa maji Juma Awesu alikuwa Naibu waziri kwenye wizara hiyo.

Nimefuatilia ziara za mawaziri hawa mikoani na kushuhudia wakipiga mikwara mizito kusimamisha kazi na kutumbua kana kwamba wao ni mawaziri wapya kwenye wizara zao.

Ndio najiuliza ni kutafuta kiki au kukosekana wapinzani ni tatizo?

Maendeleo hayana vyama!
Biteko wa madini pia
 
Back
Top Bottom