Tumbua tumbua inayofanywa na mawaziri Jafo na Aweso ni kama vile hawakuwepo kwenye Wizara hizo!

Tumbua tumbua inayofanywa na mawaziri Jafo na Aweso ni kama vile hawakuwepo kwenye Wizara hizo!

Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo siyo mgeni wizarani hapo amekuwepo tokea muhula wa kwanza wa Rais Magufuli kadhalika Waziri wa maji Juma Awesu alikuwa Naibu waziri kwenye wizara hiyo.

Nimefuatilia ziara za mawaziri hawa mikoani na kushuhudia wakipiga mikwara mizito kusimamisha kazi na kutumbua kana kwamba wao ni mawaziri wapya kwenye wizara zao.

Ndio najiuliza ni kutafuta kiki au kukosekana wapinzani ni tatizo?

Maendeleo hayana vyama!
Ndivyo ilivyo bwashee!

Hata yule anayesema tumeibiwa sana na yeye alikuwepo tangu miaka ya 2000s kwenye Serikali lakini hakuwahi kusema chochote
 
Watendaji watawakumbuka Chadema maana walikuwa ndio sehemu ya kutafutia kiki hawa mawaziri.

Nadhani hata bunge " litadoda" sana!

Maendeleo hayana vyama!
Nafikiri bunge la chama kimoja mali linaweza kuwa challenging tu.
Kumbuka G55.
 
Hii awamu ya tano kiongozi bila kutumbua anajiona hajafanya kazi, wamegeuza hicho kitendo kimekuwa cha kawaida kama fasheni, wasiwasi wangu wasiwaonee tu hao wanaowatumbua.
uswahilini tunasema anacheza na mdundo wa muziki tu...kama ni singeli basi atavua shati au kama ni bolingo basi atachomekea shati ndo maisha hayo
 
kiufupi inakera sana hata sikhizi unakuta mtu ni kweli ametenda kosa lakini jinsi litakavowekwa na kupambwa hapo mmhh unajiuliza ni kweli tumefikia kwenye ubnadamu huu...chukulia ishu ya mbunge aliyeshindwa kuapa..yaani anatumbuliwa kisa alishindwa kuapa
 
Aina ya wabunge wa 1990s ni tofauti kabisa na hawa chumia tumbo wa leo bwashee!
Watakua tu mkuu, na kuota meno.
Sayansi ya siasa(political science) inagusa kila fani y maisha ya binadamu, uwe umeelika au huja elimika.
Discussions , agreements, disagreements kutokana na thought, vimekuweo toka Adam na Hawa.

Wale wasomi wanaenda mbali zaidi:
Political science is methodologically diverse and appropriates many methods originating in psychology, social research and cognitive neuroscience. Approaches include positivism, interpretivism, rational choice theory, behaviouralism, structuralism, post-structuralism, realism, institutionalism, and pluralism.
 
Hii awamu ya tano kiongozi bila kutumbua anajiona hajafanya kazi, wamegeuza hicho kitendo kimekuwa cha kawaida kama fasheni, wasiwasi wangu wasiwaonee tu hao wanaowatumbua.
Sishangai watumishi kutumbuliwa,hasa Wizara ya Maji,ni wazembe mno na wengi wanafanya kazi kwa mazoea,weledi hamna.Kwa upande wa Aweso yeye kutumbua ni sawa,si alikuwa Naibu Waziri,so he was dancing to the tune of his boss.Muache kijana apige kazi wananchi wapate huduma bwana,tusianze kumkatisha tamaa,bora asionee kama ulivyo-sema.
 
Nchi ilijaa uzembe acha vitembee viboko,tumbua tumbua na kusweka ndani mpaka tabia zinyooke!! Kazi serikalini zilizembewa sana sasa bado walimu,wengi niwazembe,watoro,hawajiandai kisa mwajiri hayuko karibu ili kumshurutisha!! lkn dawa yao inachemka wao nikudai nyongeza na madaraja kutwa kucha... Ngojaaaa tutawanyosha kimfumo!!
 
Back
Top Bottom