PreGE2025 Tume huru INEC yataja vigezo sita kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
INEC imetangaza vigezo sita kwa asasi na taasisi za kiraia zenye nia ya kutoa elimu

1745518436240.jpeg

Mkurugenzi wa INEC Tanzania Bw. Ramadhani Kailima
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza vigezo sita kwa asasi na taasisi za kiraia zenye nia ya kutoa elimu ya mpiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima, amesema taasisi inapaswa kuwa imesajiliwa kisheria, iwe imefanya kazi halali nchini kwa angalau miezi sita, na kati ya viongozi wake watatu wakuu, wawili lazima wawe Watanzania endapo kuna viongozi wa kimataifa.

Pia, taasisi yoyote iliyowahi kuhusishwa na uchochezi au kuvuruga amani haitaruhusiwa kushiriki. Taasisi inapaswa kuwa na uzoefu katika kutoa elimu ya mpiga kura na iwe na uwezo wa kifedha kujigharamia bila kutegemea INEC.

Masharti mengine yanataka maombi yaambatane na nakala ya cheti cha usajili, katiba ya taasisi, majina ya viongozi watatu wa juu, anuani ya makazi na mawasiliano ya taasisi.

Maombi yanapokelewa hadi Mei 20, 2025. INEC imesisitiza umuhimu wa elimu ya mpiga kura kutolewa kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria, ili kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye uchaguzi
 
INEC imetangaza vigezo sita kwa asasi na taasisi za kiraia zenye nia ya kutoa elimu

View attachment 3314459
Mkurugenzi wa INEC Tanzania Bw. Ramadhani Kailima
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza vigezo sita kwa asasi na taasisi za kiraia zenye nia ya kutoa elimu ya mpiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima, amesema taasisi inapaswa kuwa imesajiliwa kisheria, iwe imefanya kazi halali nchini kwa angalau miezi sita, na kati ya viongozi wake watatu wakuu, wawili lazima wawe Watanzania endapo kuna viongozi wa kimataifa.

Pia, taasisi yoyote iliyowahi kuhusishwa na uchochezi au kuvuruga amani haitaruhusiwa kushiriki. Taasisi inapaswa kuwa na uzoefu katika kutoa elimu ya mpiga kura na iwe na uwezo wa kifedha kujigharamia bila kutegemea INEC.

Masharti mengine yanataka maombi yaambatane na nakala ya cheti cha usajili, katiba ya taasisi, majina ya viongozi watatu wa juu, anuani ya makazi na mawasiliano ya taasisi.

Maombi yanapokelewa hadi Mei 20, 2025. INEC imesisitiza umuhimu wa elimu ya mpiga kura kutolewa kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria, ili kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye uchaguzi

Kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.

Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.

Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT
 
Maandishi tu hayo, utaambiwa kafungue kesi mahakamani, ukienda mambo ya online , na mwisho mahakama imetupa maombi yako. Ukikata rufaa 2026 mahakama inaweza kukupa ushindi lkn too late uchaguzi umeisha
 
Kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.

Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.

Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT
Japo linahitaj ufafanuzi zqidi, je what happens pale jamihuri inapovunjansheria zake?
 
Mkuu, shukrani kwa kutupa shule kuhusu ubatili wa INEC, sasa wanashupaza watasimamia uchaguzi uwe huru na pia Waziri Mkuu anasema INEC watausimamia uchaguzi uwe huru na wa haki !
 
Hizo ni Ghiriba tu za kiutawala.

Tume ni batili na wala siyo huru, Je, huo Uchaguzi wa huru na Haki utatoka wapi?
Je, inawezekana vipi nyoka kuzaa tembo?
Daima, Mwana wa nyoka ni nyoka, na mwana wa tembo ni tembo! Not otherwise.

Hizo ni Ghiriba za Watawala Madikteta, kama vile wafanyavyo Watawala Madikteta wa kule Korea ya Kaskazini kwa kuiita Nchi hiyo eti kuwa ni Jamhuri ya 'Kidemokrasia' ya Korea ya Kaskazini wakati kwenye nchi hiyo hakuna kabisa hata chembe chembe za kuwepo kwa harufu ya demokrasia!
 
Uchaguz upi sasa

Na huyo mpiga kura anaye enda kupiga kura ni nani sasa mjinga huyo
 
Back
Top Bottom