INEC imetangaza vigezo sita kwa asasi na taasisi za kiraia zenye nia ya kutoa elimu
View attachment 3314459
Mkurugenzi wa INEC Tanzania Bw. Ramadhani Kailima
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza vigezo sita kwa asasi na taasisi za kiraia zenye nia ya kutoa elimu ya mpiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima, amesema taasisi inapaswa kuwa imesajiliwa kisheria, iwe imefanya kazi halali nchini kwa angalau miezi sita, na kati ya viongozi wake watatu wakuu, wawili lazima wawe Watanzania endapo kuna viongozi wa kimataifa.
Pia, taasisi yoyote iliyowahi kuhusishwa na uchochezi au kuvuruga amani haitaruhusiwa kushiriki. Taasisi inapaswa kuwa na uzoefu katika kutoa elimu ya mpiga kura na iwe na uwezo wa kifedha kujigharamia bila kutegemea INEC.
Masharti mengine yanataka maombi yaambatane na nakala ya cheti cha usajili, katiba ya taasisi, majina ya viongozi watatu wa juu, anuani ya makazi na mawasiliano ya taasisi.
Maombi yanapokelewa hadi Mei 20, 2025. INEC imesisitiza umuhimu wa elimu ya mpiga kura kutolewa kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria, ili kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye uchaguzi
Maandishi tu hayo, utaambiwa kafungue kesi mahakamani, ukienda mambo ya online , na mwisho mahakama imetupa maombi yako. Ukikata rufaa 2026 mahakama inaweza kukupa ushindi lkn too late uchaguzi umeishaKwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.
Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.
Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT
Japo linahitaj ufafanuzi zqidi, je what happens pale jamihuri inapovunjansheria zake?Kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.
Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.
Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT
Kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.
Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.
Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT
Mkuu, shukrani kwa kutupa shule kuhusu ubatili wa INEC, sasa wanashupaza watasimamia uchaguzi uwe huru na pia Waziri Mkuu anasema INEC watausimamia uchaguzi uwe huru na wa haki !