PreGE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yawataka wapiga kura kuhakiki taarifa zao kwa simu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka wananchi kutumia njia rahisi za kiteknolojia kuhakiki taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi ujao.

Akizungumza leo Aprili 14, 2025 na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jacobs Mwambegele, amesema wapiga kura wanaweza kuhakiki taarifa zao kwa kutumia simu ya mkononi au kutembelea tovuti rasmi ya tume.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ameongeza kuwa huduma hiyo inalenga kuhakikisha kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura anapata nafasi ya kuhakiki taarifa zake kwa wakati kabla ya uchaguzi.

Katika hatua nyingine, Mwambegele amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi na uboreshaji wa daftari.
Tume inaendelea na maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kupiga kura awamu ya pili, huku ikihimiza ushiriki wa wananchi kwa njia zote rasmi zilizowekwa.

Nikisikia neno tume halafu bila aibu huru ya uchaguzi, wanatoa maelekezo fulani huwa sioni ukweli, naona kama naibiwa tu...
 
Hii Tume ni ya Uchafuzi tunataka TUME HURU YA UCHAGUZI.

NO REFORMS NO ELECTION

Muachilieni TUNDU LISSU aendelee na kampeni zake za kuwazindua Watanzania.
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka wananchi kutumia njia rahisi za kiteknolojia kuhakiki taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi ujao.

Akizungumza leo Aprili 14, 2025 na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jacobs Mwambegele, amesema wapiga kura wanaweza kuhakiki taarifa zao kwa kutumia simu ya mkononi au kutembelea tovuti rasmi ya tume.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ameongeza kuwa huduma hiyo inalenga kuhakikisha kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura anapata nafasi ya kuhakiki taarifa zake kwa wakati kabla ya uchaguzi.

Katika hatua nyingine, Mwambegele amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi na uboreshaji wa daftari.
Tume inaendelea na maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kupiga kura awamu ya pili, huku ikihimiza ushiriki wa wananchi kwa njia zote rasmi zilizowekwa.

Kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.

Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.

Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT
 
Back
Top Bottom